Pata taarifa kuu
IRAN

Matokeo ya uchaguzi wa Uraisi Iran yangojewa kwa hamu

Raia nchini Iran wanayasubiri matokeo ya uchaguzi uliofanyika ijumaa kwa hamu na gamu ambayo huenda yakawa tayari kutangazwa baadaye baada ya muda wa zoezi la kupiga kura kuongezwa kwa masaa matano zaidi.

Zoezi la kupiga kura nchini Iran lilijiri ijumaa 14 june 2013.
Zoezi la kupiga kura nchini Iran lilijiri ijumaa 14 june 2013. REUTERS/Fars News/Mohammad Akhlagi
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wanaosimamia uchaguzi walilazimika kuongeza muda wa zoezi hilo kukamilika baada ya kushuhudia misururu mirefu ya wapiga kura wakiwa vituoni mpaka wakati wa usiku.

Matokeo ya awali yanatarajiwa baadaye ambapo mshindi atachukua nafasi ya rais Mahmoud Ahmadinejad anayemaliza mihula miwili baada ya kuwa mamlakani kwa kipindi cha miaka minane iliyoshuhudia matatizo ya kiuchumi na vikwazo kutoka kwa mataifa ya magharibi dhidi ya mpango tata wa Iran kuhusu Nyuklia.

Wagombea sita wamewania kiti hicho huku watano wakielezwa kuwa wasiopenda mabadiliko isipokuwa Hassan Rowhani, ambaye amepokea uungwaji mkono katika siku za hivi karibuni kutoka kwa marais wa zamani.

Uungwaji mkono wa Rowhani, uliongezeka baada ya Mohammad Reza Aref kujiondoa baada ya kushawishiwa na waliokuwa wakati mmoja marais wa nchi hiyo Mohammad Khatami na Akbar Hashemi Rafsanjani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.