Pata taarifa kuu
TANZANIA-CHINA

Rais wa China, Xi Jinping ameahidi nchi yake kushirikiana na Tanzania

Nchi ya Tanzania na China zimetiliana saini mikataba kumi na saba ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili itakayoshuhudia kuimarika kwa uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili. 

Rais wa China, Xi Jinping akiwa na mwenyeji wake rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa China, Xi Jinping akiwa na mwenyeji wake rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mikataba hiyo imetiwa saini wakati wa ziara ya rais wa China nchini Tanzania, Xi Jinping ambaye aliwasili siku ya Jumapili ikiwa ikiwa ni zaira yake ya pili akitokea nchini Urusi ambako alianzia ziara yake.

Mbali na kutiliana saini mikataba ya kibiashara, nchi hizo pia zimesaini mikataba ya kimaendeleo hasa kwenye sekta ya elimu, afya, utamaduni na miundo mbinu.

Ziara ya Jinping nchini Tanzania inaelezwa kuwa ya umuhimu kwa nchi hizo mbili, ambapo nchi ya China ni ya pili kwa kuwa na uwekezaji mkubwa nchini humo ambapo imewekeza kwenye kilimo, madini na viwanda ambapo imekuwa ikitoa mchango mkubwa kwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa ziara ya rais Jinping barani Afrika inaendelea kutuma ujumbe mzito kwa mataifa kama ya Marekani na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kuhusu ushirikiano wa nchi ya China na bara hilo ambapo uwekezaji wake umeshuhudia China ikipata faida ya zaidi ya dola bilioni 113 kwa mwaka uliopita.

Rais Xi Jinping ameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kati ya nchi yake na Tanzania na kuahidi misaada zaidi kwa nchi hiyo ambapo pia ameeleza mikakati ya nchi yake kuhusu kuendelea kushirikiana na vongozi wa bara la Afrika katika shughuli za kimaendeleo.

Kiongozi huyo siku ya Jumatatu anatarajiwa kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ziara kama hiyo kabla ya kuhitimisha ziara yake kwa kuelekea nchini Congo Brazzaville.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.