Pata taarifa kuu
INDONESIA

Watu sita wameopolewa kutoka baharini wakiwa hai hii leo baada ya boti kupotea katika pwani ya Indonesia.

Watu sita wameopolewa kutoka Baharini wakiwa hai hii leo baada ya Boti iliyokuwa imebeba watu waliokuwa wakitafuta hifadhi kupotea katika pwani ya Indonesia, hata hivyo bado hakuna dalili yeyote ya kufahamu walipo watu wengine 144 waliokuwa katika Boti hiyo. 

sbs.com.au
Matangazo ya kibiashara

Meli ya Mizigo ya Bahrain imewapata manusura hao ikiwa ni muda wa takriban siku moja baada ya vikosi vya uokoaji vya Indonesia kuahirisha zoezi la uokoaji.

Hakuna uthibitisho wa kuwepo Manusura wengine waliokuwa ndani ya Boti iliyokuwa imebeba watu 150,Boti iliyopata hitilafu kwenye Injini kabla ya kupotea.

Australia imeakuwa ikikabiliwa na Changamoto ya uingiaji wa lindi la watu wanaotafuta hifadhi nchini humo ambao huwasili kwa Boti zisizo madhubuti baada ya kukimbia nchi zao.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.