Pata taarifa kuu
MEXICO

Pena Nieto ashinda Uchaguzi wa Rais nchini Mexico na kuwa Kiongozi wa kwanza kijana kushika wadhifa huo

Tume Huru ya Uchaguzi Nchini Mexico IFE imemtangaza Mgombea wa Chama Cha PRI Enrique Pena Nieto kuwa mshindi wa Uchaguzi wa rais uliofanyika siku ya jumapili na kumfanya kuwa rais kijana zaidi kuwahi kuliongoza Taifa hilo.

Rais Mteule wa Mexico Enrique Pena Nieto akiwapungia wafuasi wake baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika siku ya jumapili
Rais Mteule wa Mexico Enrique Pena Nieto akiwapungia wafuasi wake baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika siku ya jumapili
Matangazo ya kibiashara

Rais wa IFE Leondardo Valdes amemtangaza Pena Nieto kuwa mshindi kwa kufanikiwa kupata asilimia thelathini na nane ya kura zote na kumzidi mpinzani wake Andres Manuel Lopez Obrador ambaye anatoka Chama Cha PRD.

Pena Nieto mwenye umri wa miaka 45 baada ya kutajwa mshindi wa kinyang'anyiro cha uchaguzi huo wa rais alijitokeza mbele ya makao makuu ya Chama Cha PRI yaliyopo Mexico City na kuwahutubia wafuasi wake.

Pena Nieto amewaambia wafuasi wa Chama Cha PRI kuwa demokrasia imechukua mkondo wake na kuwashukuru wale wote ambao wamejitokeza na kutumia haki yao ya msingi ya kuchagua Kiongozi wanayemtaka.

Rais huyo Mteule alipokelewa na wafuasi wake kwa furaha huku wakimuimbia kwa furaha Rais! Rais! Huku mwenye akionesha utayari wake wa kuwaunganisha wananchi wote wa Mexico.

Pena Nieto hakusita kumtaka kwa jina Rais anayeondoka Felipe Alvaro Calderon na kusema amechangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa demokrasia katik nchi hiyo na hivyo kumfanya yeye kufanikiwa kushinda kwa amani na utulivu.

Pena Nieto amewataka wananchi wa Mexico kutambua kuwa kipindi cha uchaguzi kimeshakwisha hivyo ni bora wakaelekeza juhudi zao kwenye kushikamana na kuijenga upya nchi hiyo.

Kwa upande wake Mgombea wa Chama Cha PRD Lopez Obrador ambaye ameshindwa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi amekataa kukubali matokeo hayo na kusema anasubiri taarifa ya mwisho ya Tume Huru ya Uchaguzi.

Mgombea mwingine ambaye ameshiriki kwenye kinyang'anyiro hicho kutoka Chama Cha Rais Calderon cha PAN Josefina Vazquez Mota ambaye anaye ameambulia asilimia ishirini na tano ya kura zote.

Rais Mteule wa Mexico Pena Nieto anaingia madarakani akiwa na jukumu la kuhakikisha anaendeleza vita ya kupambana na magenge ya wauzaji wa dawa za kulevya ambaye imezishwa na mtangulizi wake Felipe Calderon.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.