Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Kundi la Taliban laua watu saba kwenye shambulizi la bomu huko Kabul kuadhimisha mwaka mmoja wa kifo cha Osama

Watu saba wamepoteza maisha kwenye Mashambulizi ya Mabomu ambayo yametekelezwa na Kundi la Wanamgambo wa Taliban nchini Afghanistan saa kadhaa baada ya Rais wa Marekani Barack Obama kufanya ziara na ikiwa mwaka mmoja tangu kuuawa kwa Kiongozi wa Mtandao wa Al Qaeda Duniani Osama Bin Laden.

Shambulizi la kujitoa mhanga lililotekelezwa nchini Afghanistan na Kundi la Wanamgambo wa Taliban
Shambulizi la kujitoa mhanga lililotekelezwa nchini Afghanistan na Kundi la Wanamgambo wa Taliban
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yamelenga nyumba za kulala wageni zinazotumika na raia wa kigeni wakiwemo wafanyakazi kutoka Umoja wa Mataifa UN, Umoja wa Ulaye EU pamoja na Mashirika ya Kutoa Misaada yanayohudumu katika nchi hiyo.

Washambuliaji hao wa mabomu wamefanikiwa kujipenyeza katika Mji Mkuu Kabul licha ya ulinzi mkali ambao uliwekwa kutokana na kufanyika kwa ziara ya rais Obama ambapo Vikosi vya Kujihami vya Nchi za Magharibi NATO walikuwa na jukumu la kushika doria.

Kundi la Wanamgambo wa Taliban limejigamba kupanga na kisha kutekeleza mashambulizi hayo ya mabomu na saa kadhaa baada ya Rais Obama na mwenzake wa Afghanistan Hamid Karzai kusaini makubaliano ya ahadi zitakazofanyiwa kazi baada ya kumalizika kwa vita nchini humo.

Shambulizi hilo limewashtua wananchi wa Afghanistan na kushindwa kuelewa ni kwa namna gani limetekelezwa licha ya utaalam mkuwa wa kiitelijensia ambao wanao Jeshi la Kulinda Amani Nchini Afghanistan ISAF ambalo linajukumu la kuhakikisha usalama wa nchi hiyo unakuwa wa uhakika.

Kundi la Taliban limesema shambulizi hili linalengo la kuzima kumbukumbu ya mwaka mmoja wa Kifo cha Osama Bin Laden ambacho kilitokea mwaka mmoja uliopita nchini Pakistan na kufanikishwa na Operesheni ya Makomando wa Marekani.

Taarifa ambazo zimetolewa na Msemaji wa Jeshi la Kulinda Amani Nchini Afghanistan ISAF Luteni Kanali Jimmie Cummings amesema wamefanikiwa kuwaua watu wote ambao walihusika kwenye shambulizi hilo na hivyo wamezima jaribio lao.

Licha ya kusema wamezima shambulizi lakini wameshindwa kuainisha watu walipoteza maisha ni kina nani na hivyo kuendelea kuacha utata wa usalama katika nchi hiyo wakati huu ambapo Rais wa Marekani Barack Obama akitangaza mwisho wa vita.
Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.