Pata taarifa kuu
INDIA

Nchi ya India yasema jaribio lake la kombora la masafa marefu limefanikiwa

Serikali ya India imefanikiwa kufanya jaribio lake la kombora la masafa marefu lenye uwezo wa kusafiri kwa umbali wa zaidi ya kilometa elfu tano linalotajwa kuwa na mafanikio wakati huu nchi hiyo ikiwa ni kitisho kwa washindani wao wakubwa China. 

Kombora la masafa marefu lililojaribiwa na nchi ya India
Kombora la masafa marefu lililojaribiwa na nchi ya India Reuters
Matangazo ya kibiashara

Duru za Kijeshi nchini India zimethibitisha kombora hilo lenye urefu wa mita kumi na saba aina ya Agni V limejaribiwa kutoka katika mtambo wake uliopo Mashariki mwa Jimbo la Orissa na kufanyika kwa mafanikio makubwa.

India imesema hatua hiyo imedhihirisha uwezo wa nchi hiyo kwenye suala la teknolojia na hivyo kupunguza tofauti ya utaalam baina yao na washindani wao China wanaliokuwa wanapinga jaribio hilo la kombora la masafa marefu.

Jaribio hilo limefanyika wakati ambapo mataifa mengine kadhaa yanayorutubisha Nyuklia yakinyimwa kufanya nafasi hiyo hatua ambayo inachukuliwa kuwa ni yakisiasa zaidi kuliko utekelezaji wa dhati wa kuzuia majaribio ya makombora ya aina hiyo.

Hivi karibuni Umoja wa Mataifa ulilaani jaribio la kombora la masafa marefu lililofanywa na nchi ya Korea Kaskazini licha ya kwamba jaribio hilo lilishindakana kutekelezeka.

Korea Kaskazini ilisema kuwa kombora lake la masafa Marefu lililenga kuboresha teknolojia ya nchi yake katika mfumo wa Sattelite jambo ambalo lilionekana linatishia usalama wa mataifa jirani.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa hatua ya Umoja wa Mataifa kukaa kimya kuhusu jaribio lililofanywa na India linadhihirisha wazi kuwa Umoja huo unayalenga kuyakomoa baadhi ya mataifa na si kupiga vita matumizi ya nyuklia kwenye silaha za masafa marefu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.