Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-KABUL

Rais Karzai avishutumu vikosi vya NATO kwa kushindwa kudhibiti mashambulizi ya Taliban mwishoni mwa juma

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai amevishushia lawama nzito vikosi vya majeshi ya NATO kwakushindwa kubaini njama za wanamgambo wa Taliban waliofanikiwa kutekeleza mashambulizi kwa saa 18 mjini Kabul. 

Afghan President Hamid Karzai said his government was pressing to end divisive NATO night raids
Afghan President Hamid Karzai said his government was pressing to end divisive NATO night raids Reuters/Mohammad Ismail
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza mara baada ya vikosi vya serikali kwa kushirikiana na vile vya majeshi ya kigeni kufanikiwa kuzima jaribio la mashambulizi ya wanamgambo wa Taliban rais Karzai amejitokeza na kuvipongeza vikosi vyake.

Licha ya kukosoa mbinu za kiintelijensia zilizotumiwa na majeshi ya NATO kubaini mipango ya Taliban, rais Karzai amevipongeza vikosi hivyo na vikosi vya serikali kwa kufanikiwa kurejesha amani mjini Kabul.

Wanamgambo wa Taliban mwishoni mwa juma walivamia na kuteka majengo ambayo yanajengwa mjini Kabul na kuanza kutekeleza mashambulizi yao dhidi ya ofisi za serikali na kambi za majeshi ya kigeni pamoja na vituo vya polisi.

Rais Karzai ametaka ulinzi kuimarishwa zaidi mjini Kabul wakati huu ambapo kundi hilo limetishia kufanya mashambulizi zaidi dhidi ya ofisi za serikali na majeshi ya kigeni.

Mashambulizi hayo yamekuja wakati ambapo majeshi ya NATO na vile vikosi vya Marekani yakitangaza kuachana na doria za usiku na badala yake vitakuwa vikishiriki doria nyakati za mchana pekee.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.