Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-MAREKANI

Wanajeshi wawili wa Majeshi ya NATO wauawa nchini Afghanistan baada ya kupigwa risasi

Wanajeshi wawili wa Jeshi la Kujihami la nchi za Magharibi NATO linaloshika doria nchini Afghanistan wameuawa baada ya kupigwa risasi Kusini mwa Jimbo la Kandahar na wanajeshi wa taifa hilo.

Wananchi wa Afghanistan wakiwa kwenye maandamano ya kupinga kuchomwa kwa Quran Tukufu kulikofanywa na Majeshi ya Marekani
Wananchi wa Afghanistan wakiwa kwenye maandamano ya kupinga kuchomwa kwa Quran Tukufu kulikofanywa na Majeshi ya Marekani Reuters/Parwiz
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hao wametambulika ni raia wa Marekani ambao wapo kwenye shughuli za ulinzi wa amani chini ya Mwamvuli wa NATO walishambuliwa na wanajeshi wa Afghanistan waliokuwa nao kwenye kambi ya kijeshi.

Majeshi ya Kulinda Amani nchini Afghanistan yanayotambulika kwa jina la Vikosi vya ISAF yamethibitisha kutokea kwa mauaji hayo ambapo wameeleza mtu mmoja akiwa amevalia magwanda ya jeshi la Afghan na mwenzake akiwa kwenye mavazi ya kawaida ndiyo waliotekeleza shambulizi hilo.

Taarifa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Zhary Niaz Mohammad Sarhadi akithibitisha kutokea kwa vifo hivyo amesema raia aliyeshiriki kwenye tukio hilo alipata silaha hiyo kwa mmoja wa wanajeshi na kwa sasa anasomea ualimu.

Sarhadi ameendelea kusema wanajeshi wengine wa Marekani waliokuwa kwenye Vikosi vya ISAF walijibu shambulizi kwa kuwafyatulia risasi mwanajeshi huyo na mwalimu na kisha kupoteza maisha.

Tukio hilo limehusishwa na machafuko ambayo yamekuwa yakitokea nchini Afghanistan tangu wanajeshi wa Marekani watajwe kuchoma Quran Tukufu katika nchi hiyo kitu kilichozusha maandamano na machafuko yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya kumi.

Vifo hivyo vinafanya wanajeshi wa Marekani waliopoteza maisha kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Afghanistan tangu kuanza kwa machafuko ya kupinga kuchomwa kwa Quran Tukufu kufikia wanajeshi sita.

Wanajeshi wa Marekani waliopo kwenye Mwamvuli wa Majeshi ya Kujihami ya nchi za Magharibi NATO wapo kwenye hatari ya kiusalama tangu kutolewa kwa taarifa za wao kushiriki kwenye uchomaji wa Quran Tukufu kwenye moja ya kambi ya kijeshi.

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai aliitaka Marekani kuhakikisha inafanya uchunguzi kubaini waliohusika kwenye tukio hilo na tayari Barack Obama aliomba radhi kwa tukio lililojitokeza huko Kabul.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.