Pata taarifa kuu
AUSTRALIA

Waziri Mkuu Julia Gillard ashinda kura ya kuwa na imani naye dhidi ya Kevin Rudd

Waziri Mkuu wa Australia Julia Gillard ameshinda kura ya kuwa na imani naye au la aliyoiitisha juma lililipota na kupigwa mapema leo jumatatu katika Bunge la nchi hiyo kwa lengo la kumaliza mzozo uliokuwepo baina yake na Waziri Mkuu wa zamani Kevin Rudd.

Australia's PM retains Labor Party Leadership
Australia's PM retains Labor Party Leadership
Matangazo ya kibiashara

Mwanamke huyo wa kwanza nchini Australia kushika wadhifa wa Uwaziri Mkuu amefanikiwa kushinda kura hiyo ya siri ambayo ilikuwa inaamua hatimaye yake ya kiuongozi na kama angeshindwa basi angeenguliwa kwenye nafasi yake.

Waziri Mkuu Gillard alilazimika kuitisha kura hiyo ya kuwa na imani naye au la kutokana na kuwepo kwa hali ya mvutano baina yake na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Rudd ambaye alisema amechukua uamuzi huo kwa kuwa wananchi walipoteza imani na serikali.

Wabunge mia moja na watatu ndiyo walishiriki kwenye zoezi hilo la upigaji kura ambapo kura sabini na moja zilionesha imani kwa Waziri Mkuu Gillard huku kura nyingine thelathini na moja zikisema hazina imani na Kiongozi huyo.

Waziri Mkuu Gillard baada ya kukamilika kwa kura hiyo ya kuwa na imani naye akasema hii imedhihirisha wananchi wa taifa hilo ni wamoja na wanamalengo ya kuhakikisha wanasonga mbele na kupata maendeleo.

Gillard akaongeza kusema anawahakikishia wananchi wa Australia kuwa mchezo ambao ulikuwa unashuhudiwa kwenye ulingo wa kisiasa sasa umefikia mwisho na huu ni wakati wa kuimarisha uongozi wa Chama Cha Labor.

Kura hiyo inatajwa huenda ikawa imesitisha harakati za Rudd ambaye amekuwa akionesha kila dalili ya kutaka kurejea kwenye wadhifa wa Uwaziri Mkuu ambao aliupoteza kwa Gillard kwenye uchaguzi uliopita.

Wachambuzi wa siasa wanasema kura hii inaweza ikakata mzizi wa fitina ambao umekuwepo tangu Rudd alipotangaza kuacha wadhifa wa Uwaziri wa Mambo ya Nje na kisha kuingia kwenye malumbano na Waziri Mkuu Gillard.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.