Pata taarifa kuu
CAMBODIA

Mahakama kuu nchini Cambodia yamuhukumu kifungo cha maisha jela, Kaing Guek Eav kiongozi wa zamani wakati wa utawala wa Khmer Rouge

Mahakama kuu nchini Cambodia imemuhukumu kifungo cha maisha jela kiongozi wa zamani wa nchi hiyo wakati wa utawala wa Khmer Rouge, Kaing Guek Eav.

Kaing Guek Eav, kiongozi wa zamani wakati wa utawala wa Khmer Rouge ambaye amehukumiwa kifungo cha maisha jela
Kaing Guek Eav, kiongozi wa zamani wakati wa utawala wa Khmer Rouge ambaye amehukumiwa kifungo cha maisha jela Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo ambaye awali mwaka 2010 mahakama hiyo ilimuhukumu kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumkuta na hatia ya kushiriki na kusimamia mauaji ya wananchi elfu kumi na tano.

Hukumu hiyo imetolewa hii leo baada ya kuwasilishwa kwa rufaa na upande wa mashtaka kupinga hukumu ya awali wakitaka kifungo hicho kuongezwa hadi kufikia kifungo cha maisha, rufaa ambayo majaji wa mahakama hiyo wamekubaliana nayo.

Akisoma hukumu hiyo jaji aliyesikiliza kesi yake, amesema kuwa kutokana na kutoridhishwa na ushaidi wa awali na kwamba hukumu iliyotolewa awali haikulingana na makosa aliyoyatenda mtuhumiwa huyo sasa imebadili kifungo hicho hadi kifungo cha maisha.

Akionekana mpole muda wote wa usomwaji wa hukumu hiyo Duch ambaye wakati wa utawala wa Khmer Rouge alikuwa ni mwalimu wa hesabu alionekana kutikisa kichwa muda wote na baadae kuchukuliwa na polisi tayari kurejeshwa rumande.

Kwa upande wao ndugu waliopoteza ndugu, wamesema kuwa wameridhishwa na hukumu hiyo ingawa haiwezi kuwarudisha ndugu zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.