Pata taarifa kuu
INDIA

Watu 16 wapoteza maisha nchini India baada ya kimbunga kuikumba pwani ya India

Watu kumi na sita wamepoteza maisha Kusini Mashariki mwa nchi ya India baada ya eneo la Pwani kukutwa na kimbunga kikali kinachosafiri kwa kasi ya kilometa mia moja na arobaini kwa saa. 

Kimbunga chaikumba pwani ya india
Kimbunga chaikumba pwani ya india Reuters/Babu
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya Majanga nchini India imesema kuwa kimbunga hicho kilichopewa jina la Thane kimeonekana kupiga zaidi eneo la Cuddalore na Jimbo la Tamil Nadu kitu kilichowafanya kuwataka wakazi kuhama mara moja.

Makamu wa Rais wa Mamlaka ya Majanga Nchini India Marri Shashidhar Reddy amesema watu hao kumi na wanne walipoteza maisha kwenye Jimbo la Tamil Nadu na wengine wawili huko Pondicherry.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.