Pata taarifa kuu
IRAQ-MAREKANI

Serikali ya Iraqi yataka wafanyabiashara wa Marekani kwenda kuwekeza katika nchi hiyo

Serikali ya Iraqi imewataka wafanyabiashara wa Marekani kwenda kuwekeza katika Taifa hilo baada ya kushuhdiwa kwa vita vya muda mrefu tangu mchakato wa kuangushwa kwa Utawala wa Marehemu Saddam Hussein.

Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Iraqi Nouri Al Maliki ndiye ametoa wito huo kwa wafanyabiashara wa Marekani akisema uwekezaji utasaidia pakubwa katika kuhakikisha uchumi wa nchi hiyo unaimarika katika kipindi kifupi.

Makutano wa Maliki na wafanyabiashara hao umekuja baada ya kufanya mazungumzo na Rais Barack Obama yenye lengo la kutamatisha uwepo wa wanajeshi elfu sita wa nchi hiyo wanaoshika doria huko Iraqi.

Waziri Mkuu Maliki amezungumza hayo akiwa kwenye ziara yake nchini Marekani katika Jiji la Washington alipokutana na wafanyabishara wakubwa katika taifa hilo kuwaeleza fursa za uwekezaji katika nchi yake.

Maliki amesema kuwa ulinzi umeimarishwa katika nchi hiyo na hivyo kwa sasa kinachotakiwa ni ushirikiano na mataifa ya kigeni katika kuruhusu uwekezaji mkubwa katika nchi hiyo ili iweze kupata maendeleo.

Kiongozi huyo wa serikali ya Iraqi amewaambia wafanyabiashara wakubwa nchini Marekani ya kwamba wanaweza kwenda kuwekeza katika sekta ya mafuta ambayo ndiyo uti wa mgongo wa nchi hiyo.

Maliki ameweka bayana kuwa licha ya uwepo wa wawekezaji kutoka mataifa ya kigeni kwenye nchi hiyo lakini bado kuna nafasi nyingi ambazo zinastahili kutumiwa kwa manufaa ya wananchi na hata wawekezaji wenyewe.

Ombi hili la wafanyabiashara wa Marekani kwenda kuwekeza nchini Iraqi linakuja wakati ambapo Majeshi ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO na hata yale ya Marekani yakiwa yamesema yataondoka nchini humo mwishoni mwa mwaka huu.

Uchumi wa Iraqi ilipata majeraha tangu majeshi ya Marekani na washirika wao Uingereza kuingia nchini humo kwa lengo la kuiangusha serikali ya Saddam Hussein wakiituhumu kumiliki silaha za maangamizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.