Pata taarifa kuu
CHINA-MAREKANI

Ushirikiano wa Marekani na China kusaidia kuimarisha Uchumi wa Dunia

Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden amemwambia mwenzake wa China Xi Jinping ya kwamba nchi hizo mbili ndizo zinazoweza kuimarisha uchumi wa dunia wakati huu ambapo ameanza ziara yake ya kikazi.

Makamu wa Rais wa Marekani Joseph Biden (Kushoto) akiwasili nchini China akiwa na mjukuu wake Naomi Biden
Makamu wa Rais wa Marekani Joseph Biden (Kushoto) akiwasili nchini China akiwa na mjukuu wake Naomi Biden Reuters路透社
Matangazo ya kibiashara

Biden ametaka uwepo wa ushirikiano wa dhati katika kushughulikia suala la kuimarisha uchumi wa dunia kwa kuwa hayo ndiyo mataifa vinara kwa kuwa na uchumi mkubwa zaidi ukilinganisha na mataifa mengine.

Ziara ya Biden imekuja wakati huu ambapo kumekuwa na ukosaji mkubwa kwa namna ambavyo Marekani inashughulikia suala lake la uchumi na hata kuzua hali ya sintofahamu nchini humo na hatimaye kuridhia kuongeza deni lake.

00:23

Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden ziarani nchini China

Makamu wa Rais wa China Jinping ambaye ndiyo mwenyeji wa Biden amesema kuwa ni matumaini ya nchi hiyo uhusiano baina yao utakuwa na watafanikiwa katika kukabiliana na hali ya uchumi ya dunia kwa sasa.

Jinping ambaye anatajwa kuwa mrithi wa Rais wa sasa wa China Hu Jintao ifikapo mwaka elfu mbili na kumi na tatu ametaka ukuaji wa haraka wa uchumi ili kukabiliana na kutetereka kwa uchumi.

Kwa upande wake Biden hakuishia hapo bali amesema wingu ambalo limetanda kwenye uchumi wao litaondoka iwapo watafanikiwa kupiga hatua za haraka kuimarisha uchumi wa dunia.

Ziara hiyo ya Biden inamkutanisha pia na Spika wa Bunge la China Wu Bangguo na kisha baadaye atakuwa na mazungumzo kwa nyati tofauti dhidi ya Rais Hu Jintao na Waziri Mkuu Wen Jiabao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.