Michezo ya Jumuiya ya Madola
Mji wa Glasgow nchini Scotland ulikuwa mwenyeji michezo ya Jumuiya ya Madola, iliyowaleta pamoja zaidi ya wanamichezo elfu nne kutoka Mataifa 71, walioshirki katika michezo 18.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Michezo hiyo ilifanyika kati ya mwezi Julai na Agosti, na kufunguliwa rasmi na Malkia wa Uingereza Elizabeth wa pili.
Mataifa ya Afrika Mashariki yaliyoshiriki katika michezo hiyo ni pamoja na Rwanda, Tanzania, Uganda na Kenya.
Uingereza ilimaliza ya kwanza ikiwa na medali 174, ikifuatwa na Australia na Canada.
Afrika Kusini ilimaliza ya saba na kuongoza barani Afrika, ikifuatwa na Nigeria huku kenya ikimaliza ya tisa duniani na ya tatu barani Afrika ikiwa na medali 25, zikiwemo 10 za dhahabu.