Pata taarifa kuu

Urusi: Uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Dagestan wavamiwa na umati wa watu

Uwanja wa ndege wa Makhachkala, mji mkuu wa jamhuri ya Urusi yenye Waislamu wengi wa Dagestan, ulifungwa Jumapili jioni Oktoba 29 baada ya kutangazwa kuwasili kwa ndege kutoka Israel. Vikosi vya usalama vimewekwa kwenye eneo hilo. Israel siku ya Jumapili iliitaka Urusi "kuwalinda raia wote wa Israeli na Wayahudi wote."

Uwanja wa ndege wa Makhachkala, mji mkuu wa Dagestan, ulivamiwa Jumapili jioni, Oktoba 29, na umati wa watu wenye chuki dhidi ya Israel, wakionekana kuwatafuta abiria wanaotoka Tel Aviv.
Uwanja wa ndege wa Makhachkala, mji mkuu wa Dagestan, ulivamiwa Jumapili jioni, Oktoba 29, na umati wa watu wenye chuki dhidi ya Israel, wakionekana kuwatafuta abiria wanaotoka Tel Aviv. AP
Matangazo ya kibiashara

"Kufuatia uvamizi wa watu wasiojulikana katikauwanja wa ndege wa Makhachkala, iliamuliwa kufunga uwanja wa ndege kwa ndege zinazowasili na kuondoka," Rossaviatsia ammesema, akiongeza kuwa vikosi vya usalama wimetumwa kwenye eneo la tukio. Kulingana na shirika la Urusi, uwanja wa ndege wa Dagestan utaendelea kufungwa hadi Novemba 6.

Kulingana na vyombo vya habari vya Izvestia na RT, watu kadhaa walivamia uwanja wa ndege na wzngine kupanda juu ya paa la jengo la uwanja wa ndege.

Video zilizochapishwa kwenye Telegram zinawaonyesha wakivunja vizuizi, wakijaribu kudhibiti magari yanayotoka uwanja wa ndege au kuvunja milango ya majengo ya uwanja wa ndege. Mojawapo ya video hizo inamuonyesha mwanamume aliyepanda kwenye moja ya mbawa za ndege ya Red Wings ya Urusi. Kulingana na tovuti maalum ya Flightradar, ndege kutoka Tel Aviv ya kampuni hii ilitua saa 7:00 usiku saa za Urusi huko Makhchkala. Kulingana na chombo huru cha habari cha Urusi Sota, ilikuwa ni safari ya ndege ambayo ilipaswa kuruka tena kuelekea Moscow saa tatu usiku.

Kabla ya kuingia kwenye kituo hicho, waandamanaji kadhaa pia walikuwa wakikagua pasipoti za watu wanaoondoka uwanja wa ndege, kulingana na picha zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii. Mmoja wao aliweza kuonekana akiwa na ango lililoandikwa: "Wauaji wa watoto hawana nafasi Dagestan."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.