Pata taarifa kuu

Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi anazuru Korea Kaskazini

Nairobi – Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergey Lavrov, amewasili nchini Korea Kaskazini, ziara inayokuja wakati huu Marekani ikieleza wasiwasi wake kuhusu uhusiano wa kijeshi unaoendelea kati ya mataifa haya vita vya Ukraine vikiendelea.

Ziara ya Lavrov katika taifa hilo la  Asia , ni ya kwanza tangu mwaka wa 2018
Ziara ya Lavrov katika taifa hilo la  Asia , ni ya kwanza tangu mwaka wa 2018 via REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Ziara ya Lavrov katika taifa hilo la  Asia , ni ya kwanza tangu mwaka wa 2018 na inatoa nafasi kwa rais Vladimir Putin kuzuru taifa hilo baada yake kuwa mwenyeji wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un jijini  Moscow mwezi moja uliopita.

Kiongozi wa Korea Kaskazini alizuru Moscow mwezi Septemba kwa mwaliko wa rais Putin
Kiongozi wa Korea Kaskazini alizuru Moscow mwezi Septemba kwa mwaliko wa rais Putin via REUTERS - KCNA

Lavrov antarajiwa kutoa maelezo kwa Korea Kasakazini kuhusu ziara ya Putin nchini China ambapo karibia viongozi kutoka mataifa 130 wanakutana kwa kongamano la tatu kuhusu uwekezaji wa China na miundo mbinu.

Aidha ziara hii pia inalenga  kujadili uwezekano wa ziara inayokuja ya Putin, kulingana na shirika la habari la serikali ya Urusi.Ziara ya Lavrov nchini Korea Kaskazini inakuja siku chache baada ya Marekani kueleza wasiwasi wake kwamba Pyongyang inaipa Moscow silaha ikiwa ni pamoja na teknolojia ya hali ya juu.

Ziara ya Sergei Lavrov nchini Korea Kaskazini inatarajiwa kutoa nafasi kuelekea ziara ya Putin nchini humo
Ziara ya Sergei Lavrov nchini Korea Kaskazini inatarajiwa kutoa nafasi kuelekea ziara ya Putin nchini humo REUTERS - EVGENIA NOVOZHENINA

Washington imedai kuwa Korea Kaskazini imetuma zaidi ya makontena 1,000 ya vifaa vya kijeshi na risasi kwa Urusi katika wiki za hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.