Pata taarifa kuu

Ukraine: Urusi yatoa hati ya kukamatwa dhidi ya Jaji kiongozi wa ICC

Urusi ilimuongeza rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Piotr Hofmanski, kwenye orodha ya watu wanaotafutwa siku ya Jumatatu, bila kutaja sababu.

Makao makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Makao makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC). REUTERS - Jerry Lampen
Matangazo ya kibiashara

Raia huyu wa Poland "anatafutwa kuhusiana na uchunguzi wa jinai," Wizara ya Mambo ya Ndani ya Urusi imesema katika hifadhidata yake ya watu wanaotafutwa, kulingana na mashirika ya habari ya serikali ya Tass na Ria Novosti.

Watu kadhaa wa ICC wanalengwa

Mnamo Machi 20, Moscow ilifungua uchunguzi wa makosa ya jinai dhidi ya mwendesha mashtaka wa ICC, Karim Khan, na majaji watatu wa mahakama hiyo ya kimataifa, siku tatu baada ya kutolewa hati ya kukamatwa dhidi ya Vladimir Putin kwa "kuwahamisha watoto kutoka Ukraine kwenda Urusi kinyume cha sheria.

Kwa hivyo, Karim Khan, mwendesha mashtaka wa ICC, analengwa kwa misingi ya "kuanzisha kesi ya jinai dhidi ya mtu asiye na hatia, pamoja na mashtaka haramu ya kufanya uhalifu mkubwa au mbaya sana", pamoja na "kutayarisha shambulio dhidi ya mwakilishi wa nchi ya kigeni”.

Ingawa Urusi sio mwanachama wa ICC, rais wa Urusi kwa hivyo anatatizwa katika safari yake ya kimataifa na tishio hili la kukamatwa. Alilazimika kukata tamaa kwenda kwenye mkutano wa kilele wa mataifa ya BRICS nchini Afrika Kusini mwezi Agosti mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.