Pata taarifa kuu

Marekani yatangaza msaada wa kijeshi wa dola milioni 345 kwa Taiwan

Rais wa Marekani Joe Biden ameidhinisha msaada wa kijeshi kwa Taiwan wenye thamani ya dola milioni 345, kulingana na Ikulu ya White House, katika hatari ya kukasirisha Beijing.

Luteka ya kijeshi mnamo Mei 30, 2019 nchini Taiwan.
Luteka ya kijeshi mnamo Mei 30, 2019 nchini Taiwan. © SAM YEH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hakuna maelezo yaliyotolewa mara moja kuhusu aina ya msaada uliotolewa, Ikulu ya White House ikizungumza Ijumaa hii, Julai 29 katika taarifa fupi kwa vyombo vya habari kuhusu "vifaa vya ulinzi" na "mafunzo ya kijeshi". Afisa wa Marekani akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, hata hivyo, alitaja mapema siku ya Ijumaa kuhusu mifumo ya uchunguzi na upelelezi, risasi na vipuri vingine na vifaa vingine vya jeshi.

Beijing inachukulia Taiwan kama sehemu ya eneo lake na inapinga kila mara kutakotolewa tangazo la msaada wa kijeshi kwa kisiwa hicho. China, ambayo inasema inapendelea kuungana tena kwa amani na Taiwan, hata hivyo, haikatai matumizi ya nguvu kufanikisha hili. Mnamo mwezi Aprili 2023, China ilifanya mazoezi ya kijeshi ya siku tatu kuzunguka kisiwa hicho kujibu kitendo cha kufanyika kwa mkutano kati ya Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Kevin McCarthy na Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen huko California.

Marekani imekuwa ikiiuzia Taiwan silaha kwa miaka mingi, lakini msaada huo mpya utatoka moja kwa moja kutoka kwa hifadhi zilizopo za Marekani, sawa na ule ambao umefanywa kwa Ukraine tangu kuanza kwa vita mwezi Februari 2022. Silaha hizi zitaiwezesha Taiwan "kuimarisha" uwezo wake wa kijeshi, sasa na katika siku zijazo", ametangaza msemaji wa Pentagon, hasa katika suala la "hifadhi [silaha] za kujihami", au hata "mfumo wa ulinzi wa anga. Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin aliashiria katikati ya mwezi Mei kwamba msaada kama huo kwa Taiwan kutoka kwa hisa za Marekani ulikuwa unazingatiwa.

Kwa mujibu wa sheria iliyopitishwa na Bunge la Marekani, imeidhinishwa kukusanya hadi dola bilioni moja katika hisa za Marekani ili kukipa kisiwa hicho kinachojitawala, kwa lengo lililowekwa la kuizuia China kwa nia yoyote ya upanuzi.

Uzinduzi mpya wa mazungumzo ya Marekani na China

Tangazo hilo kutoka Ikulu ya Marekani linakuja huku kukiwa na mazungumzo mapya kati ya Marekani na China, baada ya mfululizo wa ziara za maafisa wakuu wa Marekani mjini Beijing, akiwemo mkuu wa diplomasia Antony Blinken na, hivi karibuni, waziri wa Fedha Janet Yellen na mjume maalumu wa masuala ya hali ya hewa John Kerry. Pia tangazo hili linakuja wakati Waziri wa Ulinzi na Antony Blinken wote wako nchini Australia kwa mikutano siku ya Jumamosi na wenzao wa kisiwa hiki. Wakati wa ziara ya Antony Blinken mjini Beijing katikati ya mwezi Juni, pande hizo mbili zilishikilia misimamo yao kuhusu Taiwan, huku zikitarajia kudumisha mawasiliano ili kuzuia mvutano usizidi kuzorota na kuwa makabiliano ya kivita.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.