Watu zaidi ya 230 wamefariki katika ajali ya treni nchini India
NAIROBI – Zaidi ya watu 230 wamefariki na wengine 900 kujeruhiwa katika ajali ya treni mashariki mwa jimbo la Odisha nchini India. Treni tatu zinaaminika kugongana katika ajali hiyo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka katika kile kinachotajwa kuwa ajali mbaya zaidi ya treni kuwahi kutokea katika karne hii.
Zaidi ya magari 200 ya kubebea wagonjwa yalitumwa katika eneo la tukio katika wilaya ya Balasore, kwa mujibu katibu mkuu wa Odisha Pradeep Jena.Treni moja ya abiria inasemekana iliacha njia ya reli kabla ya kugongana na nyingine usiku wa Ijumaa.
Hii ndio ajali mbaya zaidi ya treni nchini India katika karne hii. Maofisa wanasema idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka zaidi.
Shirika la Reli la India lilisema treni mbili zilizohusika katka ajali hiyo ni Coromandel Express na Howrah Superfast Express.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi alisema amesikitishwa na tukio hilo na kutoa pole zake kwa familia zilizofiwa.
Distressed by the train accident in Odisha. In this hour of grief, my thoughts are with the bereaved families. May the injured recover soon. Spoke to Railway Minister @AshwiniVaishnaw and took stock of the situation. Rescue ops are underway at the site of the mishap and all…
— Narendra Modi (@narendramodi) June 2, 2023
Naye waziri wa mambo ya ndani Amit Shah alitaja tukio hilo kuwa la "kuumiza sana". Siku ya maombolezo imetangazwa katika jimbo hilo.