Pata taarifa kuu
UTAFITI-SAYANSI

China itatuma raia wake wa kwanza angani siku ya Jumanne

China itamtuma mwanaanga wa kiraia angani kwa mara ya kwanza katika historia yake siku ya Jumanne kwa ujumbe wa mtu kwenye kituo cha anga za juu cha Tiangong, hatua nyingine katika kutekeleza azma yake ya uchunguzi zaidi ya angahewa ya dunia.

Mwanaanga huyo raia ataruka katika obiti pamoja na kamanda wa misheni ya Shenzhou-16 Jing Haipeng na mwanaanga Zhu Yangzhu.
Mwanaanga huyo raia ataruka katika obiti pamoja na kamanda wa misheni ya Shenzhou-16 Jing Haipeng na mwanaanga Zhu Yangzhu. © AP - Li Gang
Matangazo ya kibiashara

Mwanaanga huyu, Gui Haichao, "mtaalamu wa upakiaji", ni "profesa katika Chuo Kikuu cha Aeronautics na Astronautics huko Beijing", Lin Xiqiang, msemaji wa Shirika la Usafiri wa Anga la China ametangaza Jumatatu katika mkutano na waandishi wa habari.

Hadi sasa, wanaanga wote wa China ambao wamepaa angani wamekuwa sehemu ya Jeshi la Ukombozi la Watu.

Bw. Gui atawajibika "kimsingi kwa usimamizi wa obiti ya mizigo" inayojitolea kwa majaribio ya sayansi ya anga, msemaji huyo amesema.

Mwanaanga huyo raia ataruka katika obiti pamoja na kamanda wa misheni ya Shenzhou-16 Jing Haipeng na mwanaanga Zhu Yangzhu.

Wafanyakazi hao wamepangwa kupaa kutoka kituo cha uzinduzi cha Jiuquan kaskazini-magharibi mwa China siku ya Jumanne saa 3:31 asubuhi kwa saa za China, shirika la Anga la China limesema.

Bw. Gui anatoka katika "familia ya kawaida" katika jimbo la Yunnan (magharibi), kimesema Chuo Kikuu cha Beihang, jina lingine la taasisi ambayo profesa huyo anafanyia kazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.