Pata taarifa kuu

Ufilipino: Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Maria Ressa afutiwa mashtaka ya kukwepa kodi

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel kutoka Ufilipino, Maria Ressa na tovuti yake ya mtandaoni ya Rappler wameachiliwa kwa kosa la kukwepa kulipa kodi leo Jumatano, huku mwanahabari huyo akipongeza hatua hiyo punde tu kwa "ukweli kudhihirika".

Maria  mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Rais wa zamani Rodrigo Duterte, aliyekuwa madarakani kuanzia 2016 hadi 2022, na mbinu zake za jeuri katika vita dhidi ya dawa za kulevya, ambazo zilisababisha maelfu ya vifo.
Maria mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Rais wa zamani Rodrigo Duterte, aliyekuwa madarakani kuanzia 2016 hadi 2022, na mbinu zake za jeuri katika vita dhidi ya dawa za kulevya, ambazo zilisababisha maelfu ya vifo. AP - Alexander Zemlianichenko
Matangazo ya kibiashara

Bi. Ressa, mshindi wa Tuzo ya kifahari ya Amani ya Nobel mwaka wa 2021 pamoja na mwandishi wa habari wa Urusi Dmitry Muratov, anakabiliwa na kesi nyingine tatu za uhalifu, ikiwa ni pamoja na kukutwa na hatia ya uhalifu wa mtandaoni, ambayo kwa sasa amekata rufaa, hatia ambayo adhabu yake ni takriban miaka saba jela.

Mwanahabari huyo aliyebobea mwenye umri wa miaka 59, ambaye pia ana uraia wa Marekani, alikuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Rais wa zamani Rodrigo Duterte, aliyekuwa madarakani kuanzia 2016 hadi 2022, na mbinu zake za jeuri katika vita dhidi ya dawa za kulevya, ambazo zilisababisha maelfu ya vifo.

"Leo ukweli unatawala. Ukweli unashinda," Bi. Ressa amewaambia waandishi wa habari baada ya uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ya Manila.

Mwanahabari huyo wa zamani wa CNN na tovuti ya Rappler, ambayo alianzisha pamoja, walishutumiwa kwa kutoa taarifa zisizo sahihi katika marejesho ya kodi kufuatia mauzo ya bondi kwa wawekezaji wa kigeni mwaka 2015.

"Madai haya yalichochewa kisiasa," Bi Ressa amesema leo Jumatano. "Tuliweza kuthibitisha kwamba Rappler si tapeli wa kodi."

Kesi dhidi yake ni ishara ya unyanyasaji wa vyombo vya habari huru nchini, kulingana na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Bi. Ressa na Bw. Muratov walitunukiwa Tuzo ya amani ya Nobel mnamo Oktoba 2021 na Kamati ya Nobel kwa vita vyao vya "kulinda uhuru wa kujieleza".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.