Pata taarifa kuu
UFILIPINO- USALAMA-AFYA

Ufilipino yaimarisha vita dhidi ya walanguzi wa dawa za kulevya

Mamia ya maofisa wa polisi wa ngazi ya juu nchini Ufilipino wametakiwa kujiuzulu wakati serikali ikiwa mbioni kukisafisha kikosi cha jeshi polisi kinachotuhumiwa kwa kushiriki ufisadi, baadhi ya maofisa hao wakihusishwa na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr.
Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr. AP - Aaron Favila
Matangazo ya kibiashara

Vita dhidi ya mihadarati nchini humo vilianzishwa na rais wa zamani Rodrigo Duterte, mrithi wake Ferdinand Marcos akiahidi kuendeleza mapambano hayo ya kumaliza biashara ya dawa za kulevya.

Maofisa hao karibia 300 wameombwa kujiuzulu baada ya uchunguzi kubaini baadhi yao walikuwa wanajihusisha na biashara ya mihadarati.

Kamati ya watu watano imetuliwa kuwachunguza maofisa wanaotuhimwa  kushiriki vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na maadili ya idara ya polisi nchini humo.

Hii sio mara ya kwanza hatua kama hii kuchukuliwa nchini humo, Rais wa zamani Fidel Ramos katika mwaka wa 1990 aliwataka maofisa wote waliokuwa na umri wa zaidi ya miaka 56 na amabo walikuwa wamehudumu kwa zaidi ya miaka 30 kustaafu.

Maofisa wa polisi wamewaua maelefu ya walanguzi wa dawa za kulevya na watumizi wake tangu mwaka wa 2016 japokuwa wakosoaji wa serikali wanasema watu wenye mamlaka na matajiri hawaguswi katika oparesheni hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.