Pata taarifa kuu

Japan kupeleka zaidi ya makombora 1,000 ya masafa marefu kukabiliana na tishio la China

Kufuatia mvutano unaoongezeka barani Asia tangu uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, Japan inafanya kilio chini ya uwezo wake ili kupata uwezo mpya wa ulinzi. Inaweza kupeleka makombora zaidi ya elfu moja ya masafa marefu, kujibu uvamizi unaowezekana wa China dhidi ya Taiwan, urushwaji wa makombora kutoka Korea Kaskazini na kukabiliana na ongezeko la shughuli za jeshi la Urusi katika Bahari ya Japani, limebaini Gazeti la Yomiuri Shimbun.

Kikosi cha Kujihami cha Japan wakishusha bendera ya taifa katika kambi ya JGSDF Miyako.
Kikosi cha Kujihami cha Japan wakishusha bendera ya taifa katika kambi ya JGSDF Miyako. © Issei Kato, Reuters
Matangazo ya kibiashara

Japan inataka kupeleka makombora elfu moja kusini mwa visiwa hivyo, katika kisiwa cha Kyushu lakini pia kwenye visiwa vidogo vilivyoko kilomita mia moja kutoka Taiwan. Masafa ya makombora yake ya kuzuia meli yataongezeka kutoka kilomita 100 hadi kilomita elfu. Hii itaiwezesha kufika maeneo ya pwani ya China na Korea Kaskazini.

Gazeti la Yomiuri Shimbun linaongeza kuwa ndege na meli za Japan pia zitakuwa na uwezo wa kurusha makombora mapya yanayoweza kulenga adui ardhini.

Kwenye televisheni, Waziri wa zamani wa Ulinzi wa Japan Itsunori Onodera ametangaza kwamba Japan lazima ionyeshe kwa nchi zinazojaribu kuishambulia kwamba zitaweza kujiweka kwenye mashambulizi ya nguvu. Nchi hiyo pia lazima ionyeshe ujasiri sawa na Ukraine ikiwa inataka kutegemea uungwaji mkono wa washirika wake kuitetea. Hili ni mojawapo ya mafunzo ambayo Japan lazima ichukue kutokana na vita vya Ukraine, amesisitiza Itsunori Onodera.

Mabadiliko ya Katiba

Tangu kuanza kwa mzozo wa Ulaya, Japan inapanga kuongeza mara mbili matumizi yake ya ulinzi ili kufikia 2% ya Pato la Taifa. Bajeti ya kijeshi ya China, karibu euro bilioni 225, ni mara tano hadi sita zaidi ya ile ya Japan.

Tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, meli na ndege za China na Urusi zimekuwa zikitokea kwenye pwani ya Japan. Wakati manowari za Urusi zimerusha makombora ya ainaya makombora yanayotumiwa nchini Ukraine, China pia inaongeza shughuli zake karibu na Visiwa vya Senkaku, vinavyotawaliwa na Japan lakini vikidaiwa kuwa sehemu ya ardhi ya Beijing.

Japan inategemea ulinzi wake juu ya mkataba wa usalama na Marekani. Hata hivyo, pia inatafuta kurekebisha Katiba yake ya ili kuendana na mabadiliko ya hali ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.