Pata taarifa kuu
INDIA- GUJARAT- BOTAD

India: 42 wafa baada ya kunywa pombe yenye sumu

Polisi nchini India imedhibitisha vifo vya watu 42 wakati wengine zaidi ya 100 wakiwa wamelazwa hosipitalini magharibi mwa taifa hilo baada yao kunywa pombe yenye sumu.

Duka la kuuza vile nchini India
Duka la kuuza vile nchini India © Murali Krishnan
Matangazo ya kibiashara

Mamia ya watu waliaanza kuuguwa mapema wiki hii baada ya kubugia pombe inayokisiwa kuwa na kemikali ya methanol katika wilaya ya Gujarat, Mamlaka kwenye eneo hilo tayari zikiwa zimeanzisha oparesheni dhidi ya aina hiyo ya pombe.

Polisi imesema watu 31 wamefariki katika wilaya ya Botad baada ya kuathirika na pombe hiyo wengine 11 wakifariki katika wilaya nyengine ya Ahmedabad jirani na Botad.

Watu 97 wamelazwa hosipitalini wakiendelea kupokea matibabu wawili kati yao wakisemakana kuwa katika hali mbaya.

Gujarat, nyumbani kwa waziri mkuu Narendra Modi, ni mojawapo ya majimbo ambayo hayaruhusu uuzaji na unywaji wa pombe.

Mamlaka katika jimbo hilo imetekeleza oparesheni kali katika baadhi ya maduka ya kuuza vileo ambapo pia baadhi ya wahudumu wamekamatwa.

Mamia ya raia huripotiwa kufariki nchini India kila mwaka kutokana na unywaji wa pombe ya bei ya chini inayotengenezwa bila ya kuzingatia vigezo.

Kati ya lita bilioni tano ya pombe inayonyweka nchini India, asilimia 40 huwa imetengenzwa bila kuzingatia kanuni na usalama wa kutengeneza bidhaa hiyo.

Pombe hiyo hutia  kemikali ya methanol kama njia ya kuongeza makali yake na iwapo itatumika na binadamu kwa mara nyingi husababisha upofu, kuharibika kwa figo au hata kifo.

Mwaka wa 2021, watu 98 walifariki kaskazini mwa mkoa wa Punjab baada ya kubugia pombe hatari.

Zaidi ya watu 150 waliripotiwa kufariki mwaka wa 2019 kaskazini mashariki mwa jimbo la Assam baada yao pia kunywa pombe mbaya, wengi wao wakiwa ni watu waliokuwa wanafanya kazi ya kuchuna majani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.