Pata taarifa kuu

Sergei Lavrov azuru Beijing kwa mara ya kwanza tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine

Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Urusi wanakutana Jumatano, Machi 30, kwa mara ya kwanza tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Wang Yi amempokea Sergei Lavrov huko Anhui, mashariki mwa China, ambapo mkutano wa tatu wa kila mwaka wa nchi jirani za Afghanistan utafanyika Alhamisi wiki hii. Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi amekaribisha matarajio ya utaratibu "wa haki" zaidi duniani, kutokana na ushirikiano wa Urusi na China.

Picha hii iliyowapigwa Machi 30, 2022 kutoka kwa video ya televisheni kuu ya serikali ya China (CCTV) kupitia AFPTV, inamuonyesha Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov (kushoto) akiwa na mwenzake wa China Wang Yi katika ziara yake ya kwanza nchini China tangu Moscow ilipoanzisha uvamizi wake Ukraine mwezi Februari, huko Huangshan katika jimbo la Anhui nchini China.
Picha hii iliyowapigwa Machi 30, 2022 kutoka kwa video ya televisheni kuu ya serikali ya China (CCTV) kupitia AFPTV, inamuonyesha Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov (kushoto) akiwa na mwenzake wa China Wang Yi katika ziara yake ya kwanza nchini China tangu Moscow ilipoanzisha uvamizi wake Ukraine mwezi Februari, huko Huangshan katika jimbo la Anhui nchini China. AFP - STR
Matangazo ya kibiashara

Wang Yi na Sergei Lavrov kwa mara nyingine tena wameonekana wakishikamana bega kwa bega mbele ya waandishi wa habari. Salamu "ishara za kizuizi" kutoka enzi ya Covid kwa wanadiplomasia hawa wawili wa China na Urusi, ambao hawajaonana tangu Vladimir Putin aje kwenye Michezo ya Olimpiki ya Beijing mwanzoni mwa mwezi wa Februari. Hii ilikuwa kabla ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, hali ambayo imezua mvutano mbaya zaidi kati ya Moscow na nchi za Magharibi tangu kumalizika kwa Vita Baridi. Ushirikiano wa kimkakati "usio na kikomo" kati ya China na Urusi unachunguzwa kwa karibu.

"Uhusiano wa Urusi na China umestahimili jaribio jipya la mabadiliko ya kimataifa," Wang Yi amesema katika dakika za kwanza za mazungumzo. "China iko tayari kufanya kazi na Urusi, ikiongozwa na makubaliano muhimu ya wakuu wa nchi hizo mbili, ili kukuza uhusiano kati ya China na Urusi katika enzi mpya hadi kiwango cha juu. "

"Ukubwa" na sio tena "bila kikomo", au sivyo "bila mipaka katika mapambano ya amani, ulinzi wa usalama na upinzani dhidi ya utawala", imebainisha Televisheni kuu ya China, CGTN, kwenye ukurasa wake wa Twitter, ikinukuu afisa mwandamizi wa serikali ya China, ambaye ameongeza kuwa "ushirikiano kati China na Urusi ni kutofungamana, kutogombana na kutolenga nchi za ulimwengu tatu (nchi). "

"Tutasonga mbele na China kuelekea mpangilio wa ulimwengu wa kidemokrasia", amesema Sergei Lavrov, kulingana na maneno yaliyoripotiwa na diplomasia ya Urusi kwenye akaunti yake ya Twitter.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi pia alifanya mazungumzo na mwenzake wa Pakistan, Shah Mahmood Qureshi, mjini Tunxi. Fursa kwa Urusi kuunda shambulio jipya kwa Marekani.

"Wale ambao walijaribu kuifanya Afghanistan kuwa kitovu cha siasa za dunia sasa wanajaribu kuchukua nafasi ya Afghanistan na Ukraine," amesema. Kwa sababu Alhamisi hii, Machi 30, huko Anhui, maafisa kutoka Asia ya Kati, Qatar, Iran na nchi nyingine jirani na Afghanistan wanakutana kuratibu msaada wa kikanda, kiuchumi na kibinadamu huko Kabul.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.