Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Waziri Mkuu wa Japan aitaka India kuchukua msimamo

Katika ziara ya kiserikali nchini India wikendi hii, Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida alionyesha wazi kuunga mkono Ukraine.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akisalimiana na mwenzake wa Japan Fumio Kishida kabla ya mkutano wao huko New Delhi, Jumamosi Machi 19, 2022.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akisalimiana na mwenzake wa Japan Fumio Kishida kabla ya mkutano wao huko New Delhi, Jumamosi Machi 19, 2022. AP - Manish Swarup
Matangazo ya kibiashara

"Japani, pamoja na India, itaendelea kujaribu kumaliza vita na kutoa msaada kwa Ukraine na nchi jirani. " Kwa kauli hii, kufuatia mkutano wake na mwenzake wa India Narendra Modi katika mkutano na waandishi wa habari, Waziri Mkuu Fumio Kishida ameishinikiza India kuchukua msimamo juu ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Lakini wito huu kutoka kwa Waziri Mkuu wa Japani uliendelea kusalia bila kujibiwa Jumamosi hii, Machi 19, kwani Narendra Modi aliridhika ktoa "changamoto mpya za kijiografia". Tamko la pamoja kati ya nchi hizo mbili, hata hivyo, linazungumzia "hatua za kukabiliana na mzozo wa kibinadamu" na "kusisitiza haja ya nchi zote kutafuta kutatua migogoro yao kwa amani kwa mujibu wa sheria za kimataifa, bila vitisho, nguvu au jaribio la kutatua migogoro kwa upande mmoja kwa kutaka kubadilisha hali ilivyo”.

Urusi, mshirika wa muda mrefu wa India

Tangu kuanza kwa mzozo huo, New Delhi imejizuia kuikosoa moja kwa moja Urusi, msambazaji mkuu vifaa vya kijeshi, ambayo ndiyo kwanza imenunua mafuta kwa bei iliyopunguzwa.

Tofauti na wanachama wengine wa muungano wa "Quad" - unaojumuisha Japan, Australia na Marekani - India ilijizuia katika kura za maazimio matatu ya Umoja wa Mataifa ya kulaani operesheni ya kijeshi ya Moscow na kujitosheleza kwa kutaka kusitishwa kwa ghasia, huku ikikataa kutaja jina la mvamizi.

Kando na suala la Ukraine, Fumio Kishida na Narendra Modi walijadili muungano wao katika eneo la Indo-Pacific. Waziri Mkuu wa Japani alitangaza yen trilioni tano (EUR bilioni 38) ya uwekezaji wa Japani nchini India katika kipindi cha miaka mitano ijayo, hasa kwa ajili ya maendeleo ya treni za mwendo kasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.