Pata taarifa kuu
G7-USHIRIKIANO

Mataifa ya G7 yaitahadharisha Urusi ikiwa itaivamia Ukriane

Mataifa ya G7 yenye viwanda vikubwa duniani, yanaonya kuwa Urusi itakabiliwa vikali iwapo itaivamia Ukraine. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani na wenzake wa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Canada na Japan wameunga mkono kauli ya Rais Joe Biden kwa Rais Vladimir Putin, alipomuonya kutothubutu kuivamia Ukraine katika mazungumzo yao kwa njia ya video.

Picha ya pamoja ya mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za kundi la G7.
Picha ya pamoja ya mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za kundi la G7. AP - Phil Noble
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii imetolewa na wanadiplomasia wa nchi hizo, wakati wa kikao chao siku ya Jumapili katika mji wa Liverpool nchini Uingereza.

Mataifa yenye uchumi mkubwa, yameungana na tumetuma ujumbe mzito kwa washirika wetu lakini pia wapinzani wetu, na tumekuwa wazi kuwa, iwapo Urusi itavamia Ukraine, tutajibu vikali na kutakuwa na madhara makubwa? AmesemaLiz Truss, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza.

Urusi ambayo imekanusha madai ya mataifa ya magharibi kuwa inapanga kuivamia Ukraine mapema mwaka 2022, imeripotiwa kuwatuma wanajeshi wake kufanya mazoezi karibu na mpaka wa nchi hiyo jirani, huku ikisema mpango wa Ukraine kujiunga na majeshi ya nchi za Magharibi NATO, unatishia usalama wa nchi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.