Pata taarifa kuu
INDIA-USHIRIKIANO

Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis aalikwa kuzuru India

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi Jumamosi amemwalika Papa Francis kutembelea nchi yake, ikiwa ni ishara ya kirafiki kwa kiongozi wa Wakatolika bilioni 1.3 kutoka kwa kiongozi wa nchi yenye waumini wengi wa Kihindu.

Modi amesema amepata fursa ya kuzungumza mambo mengi na Papa alipomtembelea kwenye makaazi yake mjini Vatican.
Modi amesema amepata fursa ya kuzungumza mambo mengi na Papa alipomtembelea kwenye makaazi yake mjini Vatican. Handout VATICAN MEDIA/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Nilikuwa na mazungumzo mazuri sana na Papa Francis. Nilipata fursa ya kujadili naye masuala mengi na pia nimemwalika kuzuru India, "Bwana Modi ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter baada ya mkutano wake na Papa Francis.

Mwaliko huo ameutoa baada ya kukutana na Papa Francis kwa mara ya kwanza, pembezoni mwa mkutano wa kilele wa viongozi wa kundi la nchi zilizostawi na zinazoinukia kiuchumi za G20, mjini Rome.

India nchi yenye waumini wengi wa Kihindu, ina takriban Wakristo milioni 28. Kabla ya mkutano wa viongozi hao wawili, redio ya Kanisa Katoliki iliripoti kuwa maombi ya awali yaliyotolewa na Vatican kutaka Papa aizuru India, yalikataliwa na nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.