Pata taarifa kuu
JAPAN-SIASA

Japan: Waziri Mkuu Yoshihide Suga kuondoka madarakani

Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga hatapeperusha bendera ya chama chakecha PLD wakati wa uchaguzi uliopangwa kufanyika Septemba 29, na ameamua kuondoka madarakani, naibu kiongozi wa chama cha PLD ametangaza leo Ijumaa.

Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga.
Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga. Philip FONG POOL/AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Bw Suga, "amesema anataka kuweka jitihada zake katika mapambano dhidi ya Corona na hatoweza kushiriki katika uchaguzi" kwa tiketi ya chama cha PLD, "amesema Toshihiri Nikai, na kuthibitisha taarifa za vyombo vya habari nchini Japan.

"Kwa kweli tangazo hililimenishangaza," Nikai ameongeza. "Inasikitisha. Alifanya kilio chini ya uwezo wake lakini baada ya kutafakari, amechukua uamuzi".

Taarifa hii haikuwa inatarajiwa sana, kwani Bw. Suga, 72, alikuwa hadi sasa anapewa nafasi kubwa ya kushinda katika uteuzi wa kuwania tiketi ya chama cha PLD katika uchaguzi mkuu.

Bw. Suga alijikuta umaarufu wake umeshuka kwa kiwango cha juu kwa muda wa miezi kadhaa kwa ajili ya usimamizi wake uliokosolewa kwa kukabiliana na janga la COVID-19, na kwa msimamo wake kusisitiza michezo ya Olimpiki ya ichezwe Tokyo, licha ya upinzani wa wananchi wengi wa Japan.

Yoshihide Suga aliingia madarakani mwezi Septemba mwaka 2020, akichukuwa mikoba ya Shinzo Abe, ambaye alijiuzulu ghafla kwa sababu za kiafya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.