Pata taarifa kuu
UTURUKI

Uturuki: Idadi ya vifo kufuatia mafuriko yaongezeka hadi 44

Watu wasiopungua 44 wamefariki dunia kufuatia mafuriko yaliyotokea eneo la Bahari Nyeusi nchini Uturuki ambapo waokoaji wanaendelea kutafuta watu ambao hawajulikani waliko.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akizuru maendeo yaliyo athirika na mafuriko huko, Bozkurt, katika jimbo la Bahari Nyeusi kaskazini mwa nchi, Agsoti 13.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akizuru maendeo yaliyo athirika na mafuriko huko, Bozkurt, katika jimbo la Bahari Nyeusi kaskazini mwa nchi, Agsoti 13. AFP - MURAT CETINMUHURDAR
Matangazo ya kibiashara

Hili ni janga la pili la asili kutokea nchini Uturuki kwa kipindi cha mwezi mmoja na mafuriko mabaya zaidi katika miaka ya hivi karibuni.

Picha zilizopigwa na shirika la habari la Reuters zinaonyesha uharibifu mkubwa katika mji wa Bozkurt ambapo timu za uokoaji zinatafuta miili ya watu iliyokwama chini vifusi vya nyumba.

Katika jengo lililoporomoka kando ya kingo za mto, watu 10 bado wanaaminika kuwa wamekwama. Maji yanaonekana yamesomba misingi ya majengo mengine kadhaa ya ghorofa.

Ndugu wa watu ambao hawajulikani waliko wanasubiri habari kuhusu wapendwa wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.