Pata taarifa kuu
INDIA

Mgogoro wa kiafya nchini India: Hopitali zaelemewa kwa idadi kubwa ya wagonjwa

India inabaini kwamba inakabiliwa na janga baya la COVID -19 wakati mlipuko wa pili unaendelea kusababisha vifo na maambukizi zaidi nchini humo. Hospitali zinakabiliwa na haba wa vifaa vya matibabu na oksijeni.

Mgonjwa anayeongezwa oksijeni anaonekana ndani ya gari akisubiri kuingia katika hospitali ya agonjwa wa COVID-19 kwa matibabu, huko Ahmedabad, India, Aprili 26, 2021.
Mgonjwa anayeongezwa oksijeni anaonekana ndani ya gari akisubiri kuingia katika hospitali ya agonjwa wa COVID-19 kwa matibabu, huko Ahmedabad, India, Aprili 26, 2021. REUTERS - AMIT DAVE
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Narendra Modi ana kipaumbele kimoja tu, kushinda uchaguzi, amebaini Jean-Joseph Boillot, mchumi na mtaalamu nchini India ambaye amechapisha hivi karibuni ripoti mbalimbali kuhusiana na mamlaka nchini iNdia kushindwa kukabiliana na janga hili.

Mamalaka nchini India imeamua wagonjwa kutibiwa nyumbani baada ya hospitali.

kulingana na vyanzo vya hospitali hali hii imesababishwa na kupanda maradufu kwa bei za mitungi ya gesi na dawa nyengine muhimu zilizomo katika mikono ya walanguzi.

Usumbufu kupata majibu ya vipimo

Maabara pia zimeelemewa na inachukua mpaka siku tatu kupata majibu ya vipimo. Hali hiyo inawaweka madktari katika wakati mgumu wa kupima hali ya maendeleo ya mgonjwa.

India imekuwa ikiripoti zaidi ya wagonjwa 300,000 kwa siku, na idadi hiyo kubwa ya wagonjwa imeuzidi uwezo wa mfumo wa matibabu nchini humo. Siku ya Jumapili pekee, watu 2,767 wamethibitishwa kufariki dunia. Hali ambayo inatia wasiwasi baadhi ya viongozi nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.