Pata taarifa kuu
TAIWAN

Biden na Suga kuonyesha mshikamano wao kwa Taiwan

Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Japani Yoshihide Suga wataonyesha umoja wao kuhusu Taiwan kwenye mkutano wa kilele Ijumaa wiki hii, kulingana na afisa mwandamizi wa utawala wa Marekani.

Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga.
Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga. AFP - MANDEL NGAN,YUICHI YAMAZAKI
Matangazo ya kibiashara

Joe Biden na Yoshihide Suga wanatarajiwa kukubaliana juu ya taarifa ya pamoja kuhusu kisiwa kinachodaiwa na China kuwa ni sehemu yake ya ardhi lakini kinachotawaliwa chini ya mfumo ya kidemokrasia, wakati wa mkutano wa kwanza wa ana kwa ana wa rais wa Marekani na kiongozi huyo wa kigeni, amesema afisa mmoja, ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Joe Biden na Yoshihide Suga pia watajadili jinsi Beijing ilivyowatendea Waislamu katika mkoa wa Xinjiang na ushawishi wake juu ya Hong Kong, wakati akitangaza uwekezaji wa dola Bilioni 2  (sawa na euro Bilioni 1.67) kutoka Japan katika mawasiliano ya 5G ili kuzuia kampuni y China ya HUAWEI.

"Mliona msururu wa taarifa kutoka Marekani na Japani juu ya mazingira ya Mlango wa Taiwan, juu ya nia yetu ya kudumisha amani na utulivu, juu ya uhifadhi wa hali iliyopo, na ninatarajia muone taarifa rasmi na mashauriano juu ya maswala haya, "afisa mkuu wa utawala wa  Biden amewaambia waandishi wa habari.

Mara ya mwisho viongozi wa Marekani na Japani kutaja Taiwan katika taarifa ya pamoja ilikuwa mwaka 1969, kabla ya Tokyo kurekebisha uhusiano na Beijing. Mpango huu sasa unakusudia kuimarisha shinikizo kwa China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.