India: Sita waangamia katika kisa cha moto katika hospitali ya Bombay
Takriban watu sita wamefariki dunia baada ya moto kuteketeza jengo moja la biashara kunakopatikana hospitali, vmamlaka katika jimbo la Mumbai, nchini India wamesema leo Ijumaa.
Imechapishwa:
Zaidi ya wagonjwa 70 waliambukiwza virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 wamehamishiwa katika hospitali zingine, afisa mmoja amesema, akiongeza kuwa uchunguzi wa kubaini sababu za tukio hilo umeanzishwa.
Haikufahamika mara moja ikiwa wagonjwa waliotibiwa COVID-19 walikuwa miongoni mwa wahanga.
Bombay ilirekodi zaidi ya kesi 5,500 Alhamisi wiki hii, rekodi kwa hilo tangu kuzuka kwa ugonjwa huo.
Idadi ya visa vya maambukizi yapindukia milioni 11.85
India imerekodi kesi mpya 59,118 za maambukizi ya virusi vya Corona kwa siku moja, ikiwa ni idadi kubwa zaidi tangu Oktoba 18, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Ijumaa na Wizara ya Afya ya India.
Idadi ya visa vya maambukizi tangu kuzuka kwa janga hilo imefikia milioni 11.85.
India imerekodi vifo 257 kutokana na janga la COVID-19 leo Ijumaa, na kufanya jumla vifo kufikia 160,949.