Pata taarifa kuu
ARMENIA-AZERBAIJAN-UFARANSA-UTURUKI-USALAMA

Macron ataka 'maelezo' kutoka Uturuki juu ya uwepo wa wanajihadi Karabakh

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameshutumu uingiliaji wa makundi ya kjihadi katika mzozo wa Nagorno-Karabakh ambao unaendelea kwa siku ya tano sasa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mkutano wa Umoja wa Ulaya huko Brussels Oktoba 1, 2020.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mkutano wa Umoja wa Ulaya huko Brussels Oktoba 1, 2020. Francisco Seco / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Emmanuel Macron anatarajia kumpigia simu rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kutaka "maelezo" kutoka kwake, rais Macron ametangaza leo Ijumaa, akitoa wito kwa Jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi, NATO, "kuwa makini" kwa vitendo vya Ankara, mwanachama wa muungano huo.

Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari katika mkutano wa Umoja wa Ulaya Alhamisi hii huko Brussels, rais wa Ufaransa alizungumzia kinaga ubaga kuhusu mgogoro unaoendelea huko Nagorno-Karabakh.

"Kulingana na taarifa zetu za kijasusi, wapiganaji 300 waliondoka nchini Syria kwenda Baku wakipitia Gaziantep [nchini Uturuki]," Emmanuel Macron amesema. Wanajulikana, walifuatiliwa, na kutambuliwa, ni wanamgambo wa makundi ya jihadi wanaoendesha harakati zao katika mkoa wa Aleppo. Kikosi kingine kinajiandaa kwenda Nagorno-Karabakh. Mstari mwekundu umevukwa, haikubaliki. "

Ufaransa, pamoja na Urusi na Marekani, ni sehemu ya OSCE "kundi la Minsk" linalohusika na kusuluhisha mzozo huu. "Nitampigia simu rais Erdogan katika siku chache zijazo kwa sababu kama mwenyekiti mwenza wa kundi la Minsk, ninafikiria kuwa ni jukumu la Ufaransa kuomba maelezo," ameongeza rais wa Ufaransa .

Mapigano yaliongezeka Alhamisi katika mkoa wa Nagorno-Karabakh licha ya wito mpya wa kusitisha mapigano. Eneo hili, ambalo lina watu wengi, raia wa Armenia, lilikuwa limejitenga na Azerbaijan, na kusababisha vita mwanzoni mwa miaka ya 1990, ambayo ilisababisha vifo vya watu 30,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.