Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya visa vya maambukizi yaongezeka Korea Kusini

Korea Kusini imerekodi kesi mpya 113 leo Jumamosi, ikiwa ni idadi kubwa zaidi tangu mwezi Machi 3. Korea Kusini pia imebaini kwamba idadi ya visa vipya vya maambukizi imeongezeka sana, na hivyo kurekodi kiwango cha juu zaidi kwa karibu miezi minne, na kesi kadhaa za watu kutoka nje ya nchi.

Korea Kusini inashuhudia mlipuko wa pili wa janga la Corona.
Korea Kusini inashuhudia mlipuko wa pili wa janga la Corona. Jung Yeon-je / AFP
Matangazo ya kibiashara

Nchi hiyo imeripoti kesi mpya 113, ikiwa ni pamoja na watu 86 waliowasili nchini kutoka nchi za kigeni, na kufanya jumla ya watu 14,092 walioambukizwa virusi vya Corona, kulingana na Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa ya kuambukia nchini korea Kusini (KCDC).

Hii ndio idadi kubwa zaidi tangu Machi 31, wakati nchi hiyo iliripoti kesi mpya 125. Pia ni mara ya kwanza korea Kusini kutangaza kesi zaidi ya 100 tangu Aprili 1.

Wasafari wanaowasili nchini Korea Kusini kutoka nchi za kigeni huwekwa karanitini kwa muda wa wiki mbili.

Mwezi Februari nchi hiyo ilikuwa kwenye nafasi ya pili kwa kuathirika zaidi na janga hilo, baada ya China ambapo ilianzia. Lakini Mamlaka nchini Korea Kusini imefanikiwa kudhibiti hali hiyo kupitia mkakati kamili wa kupima na kutafuta watu waliotangamana na watu walioambukizwa, bila hata kukazia hatua ya kupiga marufuku ya kutembea.

Kuongezeka huko kwa visa vya maambukizi kunakuja wakati nchi hiyo inatarajia kuruhusu watazamaji kuanzia Jumapili kuhudhuria michezo kwa idadi ndogo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.