Pata taarifa kuu
CHINA-HONG KONG-USALAMA

Hong Kong: Sheria tata ya usalama wa kitaifa yapitishwa China

Bunge la China limepitisha sheria tata ya usalama ya kitaifa huko Hong Kong, vyombo vya habari katika eneo hilo linalojitawala vimebaini, na kuongeza hofu ya kukandamizwa kwa upinzani wa kisiasa katika koloni hilo la zamani la Uingereza.

Makabialiano kati ya polisi na waandamanaji huko Hong Kong kupinga sheria tata ya usalama ya kitaifa. (Picha kumbukumbu).
Makabialiano kati ya polisi na waandamanaji huko Hong Kong kupinga sheria tata ya usalama ya kitaifa. (Picha kumbukumbu). REUTERS/Tyrone Siu
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo inatarajiwa kuchochea ghasia katika kitovu hicho cha kibiashara na kuongeza mvutano kati ya China na Marekani.

Hivi rais wa Marekani alitangaza kutokubaliana na sheria ya usalama wa China kwa Hong Kong ambayo imeendelea kuzusha wasiwasi mkubwa katika jimbo hilo linalojitawala.

Rais Trump alisema kuwa China imekiuka makubaliano ya uhuru wa Hong Kong kwa kupitisha sheria ya usalama wa Kitaifa. Nakala ambayo inaruhusu kurudi kwa vyombo vya usalama vya China kwa koloni la zamani la Uingereza na ambayo kwa wengi ni tishio kwa uhuru wa eneo hilo.

Jumatatu wiki hii serikali ya China ilibaini kwamba inataka kuchukuwa vikwazo vya kuwanyima visa baadhi ya maafisa wa Marekani baada ya uamuzi kama huo uliochukuliwa na Washington dhidi ya maafisa kadhaa wa Chama cha Kikomunisti cha China, na hii, ni kutokana na hatua ya Beijing kwa Hong Kong.

Kauli hiyo ilitolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Zhao Lijian, katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu Juni 29.

Sheria hiyo itawaadhibu wanaojihusisha na kutaka kujitenga, kudhoofisha nguvu ya serikali, ugaidi na vitendo vyote vinavyotishia usalama wa taifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.