Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-KOREA KUSINI-AFYA-USALAMA

Seoul: Kim Jong-un huenda anajaribu kujikinga na maambukizi ya Corona

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un hajahudhuria sherehe rasmi ya Aprili 15, sio kwa sababu ya hali yake ya kiafya, lakini kama hatua ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya janga laCovid-19, waziri mwenye dhamana ya muungano wa Korea Kusini amesema.

Uvumi kuhusu hali ya kiafya ya Kim Jong-un, kwa sehemu kubwa umesababishwa na kutoonekana kwake hadharani kwa kipindi kirefu.
Uvumi kuhusu hali ya kiafya ya Kim Jong-un, kwa sehemu kubwa umesababishwa na kutoonekana kwake hadharani kwa kipindi kirefu. Alexander SAFRONOV / Press Service of Administration of Primorsk
Matangazo ya kibiashara

Kukosekana kwa kiongozi huyo wa Korea Kaskazini wakati wa sherehe hii ya kijadi ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa babu yake Kim Il-sung, mwanzilishi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, haijawahi kutokea na hajawahi kuonekana hadharani tangu wakati huo, hali ambayo ilichochea uvumi kuhusu hali yake ya afya.

Kituo cha habari cha Daily NK, chenye makao yake mjini Seoul, ambacho kimenukuu chanzo kutoka Korea cha Kaskazini kiliripoti wiki iliyopita kwamba Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alifanyiwa upasuaji wa moyo Aprili 12.

"Ni kweli kwamba hajawahi kukosa katika sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa Kim Il-sung tangu kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi, lakini maadhimisho mengi yalisitishwa kwa sababu ya hofu kuhusu ugonjwa aw Covid-19," amesema Kim Yeon-chul, Waziri mwenye dhamana ya muungano wa China, wakati wa kikao cha wabunge.

"Sidhani kama ni kawaida sana katika hali ya sasa," Kim Yeon-chul amebaini, na kuongeza kuwa mara mbili tangu katikati ya mwezi wa Januari, Kim Jong-un hajajitokeza hadharani kwa karibu siku 20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.