Pata taarifa kuu
URUSI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa vipya zaidi ya 1,000 vya maambukizi vyaripotiwa Urusi

Urusi imetangaza visa vipya 1,154 vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19 kati ya Jumatatu na Jumanne wiki hii, na kuvuka kiwango cha juu cha watu 1,000 kwa mara ya kwanza, maafisa wa afya wamebaini.

Kwa saa 24 pekee Urusi imetangaza visa vipya 1,154 vya maambukizi ya virusi vya Corona.
Kwa saa 24 pekee Urusi imetangaza visa vipya 1,154 vya maambukizi ya virusi vya Corona. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kwa jumla, Urusi imesema watu 58 wamefariki dunia tangu ugonjwa huo kuzuka nchini humo na watu 7,497 wameambukizwa virusi vya Corona.

Siku moja baada ya daktari aliyekutana na rais Putin wiki mbili zilizopita kukapatikana na virusi vya Corona ,msemaji wa Kremlin alisema “rais wa Urusi Vladimir Putin atakuwa akifanya kazi akiwa nyumbani kwake huko Novo-Ogarevo, karibu na jiji la Moscow."

Katika kujaribu kukabiliana na kuenea kwa virusi vya Corona, hasa katika mji mkuu Moscow, ambao umekuwa kitovu cha janga nchini Urusi, hivi karibuni manispaa ya mji wa Moscow ilitangaza marufuku ya kutoka nje.

Katika chini ya miezi miwili virusi vya Corona vimesambaa hadi mabara kadhaa. Janga lina maana ya kwamba virusi hivyo vinasambaa kwa kasi ya juu katika zaidi ya mabara matatu.

Visa vya kwanza vya ugonjwa hatari wa mapafu viliripotiwa nchini China mnamo tarehe 31 mwezi Disemba 2019 na ilipofikia tarehe 7 mwezi Januari virusi hivyo tayari vilikuwa vimefichuliwa. Virusi vya Corona viligunduliwa siku 10 baadaye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.