Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-UGAIDI

Hotel ya kifahari ya Intercontinental yashambuliwa jijini Kabul

Watu watano wameuawa baada ya kupigwa risasi na wengine nane kujeruhiwa baada watu wenye silaha kuwavamia hoteli ya kifahari ya Intercontinental jijini Kabul nchini Afganistan.

Mwonekano wa hoteli ya  Intercontinental jijini Kabul Januari 21 2018
Mwonekano wa hoteli ya Intercontinental jijini Kabul Januari 21 2018 REUTERS/Mohammad Ismail
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa usalama wamekuwa wakikabiliana na wavamizi hao kwa zaidi ya saa 10 kutoka siku ya Jumamosi, baada ya kutokea kwa shambulizi hilo.

Ripoti zinasema wavamizi hao walifika katika hoteli hiyo ya kifahari na kuanza kuwafwatulia risasi watu na baadaye kuanza kuchoma moto hoteli hiyo.

Wanajeshi wa Afghanistan walifika kwa helikopta, na kuanza kukabiliana na wavamizi hao ambao walikuwa wamewateka mamia ya watu ambao tayari wameachiliwa huru.

Moshi mweusi umeendelea kufuka katika orofa ya sita ya hoteli hiyo, huku watu wakionekana wakiondoka katika hoteli hiyo ka hofu.

Wizara ya Mambo ya ndani imesema wavamizi wawili kati ya wanne waliovamia hoteli hiyo wameuawa katika makabiliano hayo.

Shambulizi kama hili, liliwahi kutokea katika hoteli hiyo mwaka 2011.

Haijafahamika waliohusika na shambulizi hili lakini inashukuwa kuwa ni wanamgambo wa Taliban.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.