Pata taarifa kuu
UTURUKI-USALAMA

Watu zaidi ya efu moja wakamatwa Uturuki

Maafisa wa usalama wamewakamata watu zaidi ya 1000 nchini kote Uturuki, watu ambao wanashukiwa kuwa wafuasi wa kiongozi wa kidini Fethullah Gülen anayeshtumiwa na rais Recep Tayyip Erdogan kuwa aliandaa jaribio la mapinduzi dhidi ya utawala wake mwezi Julai mwaka jana.

Polisi wakisindikiza watu wanaotuhumiwakuwa katika vuguvugu la Bw Gulen katika mji wa Kayseri, Aprili 25, 2017.
Polisi wakisindikiza watu wanaotuhumiwakuwa katika vuguvugu la Bw Gulen katika mji wa Kayseri, Aprili 25, 2017. Olcay Duzgun/Dogan News Agency/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Jaribio ambalo lilitibuliwa na vikosi watiifu wa rais huyo wa Uturuki. Serikali ya Uturiki inaendelea na operesheni yake ya kuwakamata wafuasi wa kiongozi huyo wa kidini aliye ukimbizi nchini Marekani.

Washukiwa wengine 2,200 walikuwa wanasakwa huku mamlaka ikisema kuwa kuna kile kinachodaiwa kuwa kikosi cha siri miongoni mwa maafisa wa polisi wa Uturuki.

Mapema mwezi huu rais wa taifa hilo alishinda kura ya maoni kuhusu kuimarisha mamlaka yake.

Kutokana na ushindi huo mwembamba rais Erdogan anaweza kuwa rais mwenye mamlaka, hatua inayomuongezea mamlaka katika wadhfa wa urais ambao haukuwa na uwezo.

Maimamu 1,009 katika mikoa 72 wamekamatwa na wanazuiliwa kufikia sasa, kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani Suleyman Soylu, ambaye aliripotiwa akiitaja kuwa hatua muhimu ya Uturuki.

Orodha ya takriban watu 3,224 ilikuwa imewekwa na maafisa wa polisi katika operesheni ya mikoa 81,r ipoti ilisema.

Katika mji mkuu wa Istanbul pekee, washukiwa 390 walikuwa wakitafutwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.