Pata taarifa kuu
UTURUKI-ELIMU

Walimu zaidi ya 10,000 wasimamishwa kazi Uturuki

Alhamisi wiki hii Serikali ya Uturuki imewasimamisha kazi walimu zaidi ya 10,000 wakituhumia kuwa na uhusiano na kundi la wapiganaji la PKK katika hali ya kamata kamata katika sekta ya elimu baada ya mapinduzi yaliyoshindwa ya Julai, afisa mmoja wa Uturuki ametangaza.

Recep Tayyip Erdogan, katika mji wa Ankara Julai 29, 2016 aendelea na operesheni yake ya kuwasimamisha kazi wafanyakazi mbalimbali wa umma. .
Recep Tayyip Erdogan, katika mji wa Ankara Julai 29, 2016 aendelea na operesheni yake ya kuwasimamisha kazi wafanyakazi mbalimbali wa umma. . REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Watu hawa wamesimamishwa muda katika majukumu yao, katika hali ya kuendesha uchunguzi," amesema kiongozi mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Jumla ya walimu 11,500 wanaotuhumiwa na Wizara ya Elimu kushirikiana katika shughuli za "kuunga mkono kundi la kigaidi na washirika wake" wamesimamishwa kazi, Shirika la habari linalounga mkono serikali la Anadolu limearifu.

Idadi inaweza kuongezeka hadi kufikia 14,000, kulingana na matokeo ya uchunguzi wa sasa, limeongeza shirika la habari la Anadolu, likithibitisha kauli ya Waziri Mkuu Binali Yildirim, aliyoitoa Jumamosi wakati wa ziara yake katika mji wa Diyarbakir (mji unaokaliwa na watu wengi kutoka jamii ya Wakurdi, kusini mashariki mwa nchi).

Operesheni hii mpya inakuja wiki moja kabla ya kuanza shule nchini Uturuki, nchi ambayo ina walimu 850,000.

Kundi la PKK, ambalo linaendelea na vita dhidi ya serikali ya Ankara tangu mwaka 1984, ambapo watu zaidi ya 40,000 waliuawa, limetajwa kuwa kundi la "kigaidi" na serikali ya Uturuki na washirika wake wa Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.