Pata taarifa kuu
AUSTRIA-UGAIDI-USALAMA

Raia wa Australia wenye asili ya kigeni waonywa

Australia imepitisha sheria ya kufuta uraia kwa raia wa Australia wenye asili ya kigeni ambao watakutikana na kosa la kushiriki katika shughuli za kigaidi, nakala ambayo inaweza kuunda "tabaka mbili za raia wa nchi hiyo".

Wahamiaji waliozuiliwa Australia, tarehe 2 Juni baada ya kutokea kwa mara ya pili Indonesia.
Wahamiaji waliozuiliwa Australia, tarehe 2 Juni baada ya kutokea kwa mara ya pili Indonesia. AFP PHOTO / Gamaliel AMALO
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Sheria wa Australia George Brandis amekaribisha uamzi wa Bunge uliochukuliwa Alhamisi usiku kuhusu sheria hii mpya ambayo inakuja, kwa mujibu wa waziri huyo, kupambana na ugaidi.

Marekebisho ya sheria hiyo yaliungwa mkono na chama cha upinzani cha Labour.

"Sheria hii itapelekea kufutiwa uraia kwa raia wa Australia wenye asili ya kigeni ikiwa watashiriki katika shughuli za kigaidi nje ya nchi au kuhukumiwa nchini Australia kwa makosa yanayohusiana na ugaidi", George Brandis amesema leo Ijumaa.

"Pia itapelekea kuzuia kurudi nchini Australia kwa magaidi wa kigeni waliopewa uraia wa nchi hiyo na kufukuzwa kwa raia wa Australia wenye asili ya kigeni ambao watajihusisha nchini Australia katika vitendo vinavyohusiana na ugaidi", ameiongeza Brandis.

Waziri George Brandis amesema mageuzi hayo ni muhimu kutokana na kiwango cha tishio la kigaidi nchini Australia na duniani kote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.