Pata taarifa kuu
URUSI-MASHAMBULIZI-UGAIDI-USALAMA

Syria: Putin aamuru meli zake "kushirikiana" na Ufaransa

Rais wa Urusi Vladimir Putin Jumanne wiki hii ameamuru meli zake za kivita ziliopelekwa katika Bahari ya Mediterranean "kuwasiliana moja kwa moja" na manuari kubwa ya kijeshi ya Ufaransa (Charles de Gaulle) na "kushirikiana na washirika wake" Ufaransa.

Mkutano wa viongozi wa kijeshi wa Urusi kuhusu operesheni za kijeshi nchini Syria, Novemba 17, 2015, Moscow.
Mkutano wa viongozi wa kijeshi wa Urusi kuhusu operesheni za kijeshi nchini Syria, Novemba 17, 2015, Moscow. LEXEI NIKOLSKY/SPUTNIK/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Kikosi cha majini kunachosafirishwa na manuari kubwakitawasili hivi karibuni katika mnalodhibiti. Mnapaswa kuwasiliana moja kwa moja na Wafaransa na kufanya kazi nao kama washirika", Vladimir Putin ametangaza katika mkutano na viongozi wa majeshiwa ya Urusi yanayoendesha operesheni za kijeshi nchini Syria.

Rais wa Urusi pia amezungumza kwa simu na mwenzake wa Ufaransa Francois Hollande kabla ya mkutano uliopangwa kufanyika Novemba 26. Viongozi hao wawili wamekubaliana "ushirikiano wa moja kwa moja" wa Idara zao za Ujasusi kuhusu mgogoro wa Syria baada ya mashambulizi ya Ijumaa katika mji wa Paris, Kremlin imesema.

Kama Ufaransa baada ya mashambulizi hayo, Urusi imeamua Jumanne hii kuongeza mashambulizi yake kutokana na ajali ya ndege ya shirika la Urusi iliyoanguka nchini Misri, ambapo Urusi hatimaye inachukulia kama shambulio la kigaidi.

Mashambulizi muhimu ya Urusi yameendeshwa kwa mara ya kwanza dhidi ya ngome za kundi la Islamic State (IS) nchini Syria, ambapo Moscow inaendesha operesheni ya kijeshi tangu Septemba 30, Waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigou amesema katika mkutano na viongozi wa kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.