Pata taarifa kuu
NEPAL-TETEMEKO-USALAMA

Juhudi za uokozi zaendelea Nepal

Idadi ya watu waliofariki nchini Nepal baada ya tetemeko la ardhi mwishoni mwa juma lililopita imefikia zaidi ya 3,000 na zaidi ya 6,000 wamejeruhiwa.

Timu za uokozi kubeba mwili wa mtalii aliyejeruhiwa baada ya kambi aliokuwemo ya Everest kuharibiwa na tetemeko Jumamosi Aprili 25.
Timu za uokozi kubeba mwili wa mtalii aliyejeruhiwa baada ya kambi aliokuwemo ya Everest kuharibiwa na tetemeko Jumamosi Aprili 25. AFP PHOTO/Roberto SCHMIDT
Matangazo ya kibiashara

Shughuli za uokoaji zinaendelea jijini Kathmandu ambapo hali inaendelea kuwa mbaya, huku Jumuiya ya Kimatifa ikiombwa kuendelea kutoa usaidizi.

Watu milioni 4.5 wamekumbwa na tetemeko hilo, ambalo ni baya zaidi kutokea nchini Nepal tangu miaka 80 iliyopita. Hali ya tetemeko ambayo imekua ikirejea mara kwa mara tangu Jumamosi mwishoni mwa jumahili lililopita katika mji wa Kathmandu imetatiza shughuli za uokoaji. Hali ni mbaya katika mji huo na huenda ikawa mbaya zaidi katika siku za usoni.

Tangu jana Jumapili idadi ya majeruhi imeendelea kuongezeka katika hospitali ya mki wa Kathmandu, na kwa sasa majeruhi wameanza kupelekwa katika hospitali za mikoani.

Jumatatu asubuhi wiki hii maelfu ya watalii bado wanasubiri katika uwanja wa ndege wa Kathmandu kwa kuweza kuondoka nchini Nepal. Uwanja wa ndege umefungwa jana Jumapili jioni kwa sababu ya hali mbaya ya hewa. Mamia ya watalii wa kigeni wamepiga kambi usiku wa Jumapili kuamkia leo Jumatatu katika vibanda vya hoteli kubwa za mji wa Kathmandu. Itakumbukwa kwamba Nepal inaishi hasa kwa utalii na maeneo ya kitalii mengi yaliharibiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.