Pata taarifa kuu
NATO-ISAF-AFGHANISTAN-Shambulio-Usalama

Shambulio la kujitoa mhanga lauawa wanajeshi 3 wa NATO

Wanajeshi watatu wa kikosi cha Umoja wa kujihami ya mataifa ya magharibi Nato wameuawa jumanne wiki hii katika shambulia la kujitoa mhanga na wengine zaidi ya 15 wamejeruhiwa katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.

shambulio la kujitoa mhanga laua wanajeshi 3 wa kikosi cha Nato nchini Afghanistan, Isaf.
shambulio la kujitoa mhanga laua wanajeshi 3 wa kikosi cha Nato nchini Afghanistan, Isaf. REUTERS/Omar Sobhani
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hao wameshambuliwa wakiwa katika msafara wa magari ya kikosi cha Isaf katikati ya mji wa Kabul. Kundi la Taliban limekiri kutekeleza shambulio hilo.

Shambulio hilo linatokea kabla ya kuondoka kwa wanajeshi wa Isaf mwishoni mwa mwezi Desemba, huku taifa hilo likiendelea kushuhudia mvutano wa kisiasa tangu kufanyika kwa uchaguzi nchini humo mwezi Juni uliyopita.

Mtu aliye jitoa mhanga ametumia gari lake ndogo ambalo limekualimebeba vilipuzi na kuliingiza kwenye msafara wa magari ya Isaf, ambao ulikua ukielekea kwenye uwanja wa ndege wa Kabul. Gari moja la kijeshi liliteketea kwa shambulio hilo, huku magari mengine 17 ya raia wa kawaida yakiharibika vibaya.

Kengele ya tahadhari kwenye ubalozi wa Marekani imelia wakati wa shambulio hilo na kupelekea eneo hilo linawekwa chini ya ulinzi mkali.

Hata hivo suala la kulinda amani nchini Afghanistan limekua ni tete, baada ya kikosi hicho cha Isaf kikijiandaa kuondoka nchini Afghanistan mwishoni mwa mwezi wa Desemba, huku mrithi wa Hamid Karzai akiwa bado hajapatikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.