Pata taarifa kuu
Bangladeshi-Maandamano

Maandamano yanaendelea nchini Bangladeshi, mtu mmoja auawa jana na polisi

Mtu mmoja ameuwa jana nchini Bangladesh baada ya Polisi kuwafyatulia risase waandamanaji wa kundi la kiislam la Jamaat-e-Islami wanaoandamana kupinga adhabu ya kifo iliotolewa dhidi ya katibu mkuu msaidizi wa kundi hilo Abdul Quader Molla aliyekutwa na hatia ya mauaji ya halaiki.

Waandamanaji nchini Bangladesh
Waandamanaji nchini Bangladesh
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Aminur Rahman mkuu wa polisi katika eneo hilo amesema Mtu huyo ameuawa wakati polisi ilipokuwa ikiwasambaratisha waandamanaji wanaokadiriwa kufikia elfu moja na mia mbili kwenye barabara kuu katika mji wa Mujibnagar magharibi mwa taifa hilo.

Waandamanaji kumi wamejeruhiwa kwenye maandamano yanayoendelea nchi nzima huko Bangladesh baada ya Jeshi la Polisi kufyatua risasi za moto ikiwa ni sehemu ya juhudi za kusambaratisha maandamano yanayoendelea kushamiri nchi nzima.

Polisi walilazimika kutimia silaha za moto katika Mji wa Mujibnagar baada ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wandamanji waliokuwa wamejihami vilivyo na fimbo za chuma huku pia wakifunga barabara.

Mkuu wa Polisi wa Mji huo Nahidul Alam amekiri kuna wafuasi wa Chama Cha Jamaat-e-Islami waliouawa kwenye makabiliano hayo pamoja na wanaharakati lakini akashindwa kuweka bayana idadi ya wale waliopoteza maisha.

Wafuasi wa Chama Cha Jamaat-e-Islami wamejiapiza kuendelea kupambana na Serikali hadi pale ambapo itafuta adhabu ya kifo dhidi ya Molla anayekutwa na hatia ya kushiriki mauaji kwenye vita vilivyozuka baada ya Uhuru mwaka elfu moja mia kenda sabini na moja.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.