Pata taarifa kuu
Bangladesh

Idadi ya watu waliokufa kutokana na kuporomoka kwa jengo Bangladesh yafikia 482

Idadi ya Waliopoteza maisha katika ajali ya kuporomoka kwa jengo lililokuwa na Kiwanda cha nguo nchini Bangladesh imefika 482 hii leo baada ya miili 41 kutolewa kutoka kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa na Ghorofa nane.Mkuu wa Operesheni ya uokoaji ameliambia shirika la habari la ufaransa kuwa idadi hiyo imeongezeka baada ya juhudi za uokoaji kufanikisha kupata miili mingine 41 usiku wa kuamikia leo.

REUTERS/Khurshed Rinku
Matangazo ya kibiashara

Jengo lililokuwa na viwanda vitano vya nguo liliporomoka karibu na mji Mkuu wa nchi hiyo, Dhaka tarehe 24 mwezi Aprili, na kusababisha takriban watu 3,000 kunasa, huku watu 2,437 wakiokolewa wakiwa hai.
 

Idadi kamili ya Watu waliopoteza maisha inatarajiwa kuongezeka na kufikia 500 baada ya Maafisa kusema kuwa watu 149 bado hawajulikani walipo.
 

Polisi nchini humo inawashikilia watu wanane akiwemo mmiliki wa Jengo hilo na Wamiliki wanne wa Kiwanda kwa kuwashurutisha Wafanyakazi kurejea kufanya kazi ndani ya jengo hilo ingawa jengo hilo lilishaanza kutoa nyufa siku moja kabla ya ajali.
 

Mamlaka nchini Bangladeshi jana ilimfukuza kazi Meya wa jimbo la Savar kwa kuidhinisha jengo hilo kutumika na kushindwa kufunga viwanda hivyo baada ya kuonekana Dosari katika Jengo hilo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.