Pata taarifa kuu
Bangladesh

Mmiliki wa jengo lililoporomoka Bangladesh, akamatwa akitaka kutoroka

Vikosi vya uokoaji vimeanza tena zoezi la uokoaji wakitumia mashine nzito nzito kusawazisha vifusi baada ya kuripotiwa Mwanamke mmoja aliyekwama kwenye kifusi cha Jengo la Ghrofa nane kupoteza maisha baada ya kuungua moto karibu na mji mkuu wa Bangladesh,Dhaka.  

REUTERS/Andrew Biraj
Matangazo ya kibiashara

Moto uliwajeruhi Wafanyakazi wa Idara ya Uokoaji takriban 6 wakati wakandarasi walipokuwa wakikata nyaya za umeme.
 

Miili zaidi inatarajiwa kupatikana wakati Wafanyakazi, wakitifua maeneo yenye vifusi kwa umakini wakihofu kuwadhuru Watu ambao pengine wako hai wakiwa wamenaswa katika Vifusi hivyo.
 

Takriban Watu 2500 wameokolewa kutoka kwenye eneo la ajali mpaka sasa huku idadi ya waliopoteza maisha ikifikia 381.
 

Katika hatua nyingine mmiliki wa Jengo lililoporomoka amekamatwa mapema siku ya Jumapili alipokuwa akijaribu kutoroka nchini humo, Waziri wa Serikali za mitaa Jahangir Kabir Nanak amethibitisha.
 

Mmiliki huyo, Sohel Rana, Mwanasiasa kupitia Chama tawala nchini humo, Awami League Party alikamatwa katika eneo la mpaka kati ya Bangladeshi na India, na kurejeshwa mjini Dhaka kwa ajili ya kuhojiwa.
 

Rana ameshutumiwa kutumia vifaa visivyo na viwango katika ujenzi wa Ghorofa hilo ambalo lililmalizika mwaka 2006.
 

Wamiliki wa Kiwanda kilichokuwa kwenye jengo hilo wanashutumiwa kupuuzia maonyo yaliyokuwa yakitolewa na Maafisa siku moja kabla ya Jengo kuanguka kuwa Jengo hili lilikua na nyufa.
 

Polisi imesema kuwa Wakurugenzi wa Kiwanda hicho waliwalazimisha Wafanyakazi kuendelea na kazi ndani ya Jengo hilo ingawa walifahamu kuwa Jengo hilo lilikuwa na nyufa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.