Pata taarifa kuu
KOSOVO

Mahakama yatupilia mbali mashtaka ya uhalifu wa kivita dhidi ya kiongozi wa zamani wa Kosovo

Mahakama ya kivita ya Umoja wa Mataifa imetupilia mbali mashtaka ya uhalifu wa kivita yaliyokuwa yanamkabili waziri mkuu wa zamani wa Kosovo Ramush Haradinaj.

(Photo : Reuters)
Matangazo ya kibiashara

Kwa mara nyingine tena mahakama hiyo imemsafisha Ramush Haradinaj pamoja na washtakiwa wenzake Idriz Balaj na Lahi Brahimaj katika mashtaka yote yaliyokuwa yanawakabili.

Jopo la majaji walioamua kesi hiyo limebaini kuwa hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kuwa watatu hao walishiriki katika kuwatesa na kuwaua waserbia katika vita vya kudai uhuru kati ya mwaka 1998 mpaka mwaka 1999.

Uamuzi huo umewaepusha na adhabu ya kifungo cha miaka 20 ambayo ilipendekezwa dhidi yao na waendesha mashtaka.

Katika upande mwingine uamuzi huo umepokelewa kwa hasira na viongozi wa Serbia na Rais wa nchi hiyo Tomislav Nikolic amesema mahakama hiyo haijatenda haki na hatua hiyo inagandamiza haki ya raia walioteswa katika mapigano hayo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.