Pata taarifa kuu
AUSTRALIA

Nchi ya Australia kwenye tahadhari ya kukumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha

Hali ya wasiwasi imeendelea kutanda nchini Australia kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini humo na kusababisha hali ya taharuki kwa wananchi wa miji mingi nchini humo.

Nyumba za mjini Brisbane Australia zikiwa zimefunikwa kabisa na maji
Nyumba za mjini Brisbane Australia zikiwa zimefunikwa kabisa na maji Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mvua kubwa iliyonyesha jana kwenye mji wa Sydney ilisababisha hali ya wasiwasi na hofu kwa wananchi kufuatia serikali kulazimika kufunga baadhi ya huduma za kijamii kama usafiri wa majini na anga kwa lengo la kuzua ajali zinazoweza kutokea kutokana na mvua hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kitengo cha hali ya hewa nchini humo imeeleza kuwa mvua hizo zimesababisha madhara kwenye baadhi ya mji wa Sydney na kutoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini katika kipindi hiki cha mvua.

Ni hivi juzi tu waziri mkuu wa Australia Julia Gilard alitangaza hali ya hatari kwenye miji ya Queensland kutokana na kuendelea kunyesha kwa mvua ambazo zimesababisha kuharibika kwa baadhi ya miundombinu.

Wananchi wa jiji la Sydney walijikuta wakikosa huduma ya simu na umeme kwa muda kutokana na kuzimwa kwa mitambo inayoongoza vyombo hivyo ikiwa ni hatua za awali kuchukua tahadhari dhidi ya maafa yanayoweza kujitokeza.

Mamlaka hiyo ya hali ya hewa imerekodi kiwango hicho cha mvua ya zaidi ya mililita 119 kuwa ni kiwango kikubwa zaidi kuwahi kunyesha kwenye mji huo toka mwaka 2007.

Zaidi ya wananchi elfu moja wameambiwa kuyahama makazi yao kwenye mji wa Forbes ambao unatarajiwa kukumbwa na mafuriko.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.